Njia za Kupata Programu za Bure Kwaajili ya Kompyuta Yako

Kama untafuta programu kwaajili ya kompyuta yako
Programu za Bure Programu za Bure

Najua kuna wakati mtu unatafuta programu flani kwa ajili ya kompyuta yako na wakati huo huo unakuta programu hiyo inauzwa bei ghali kiasi kwamba huwezi kuipata kwa wakati unayohitaji, kukusaidia kataika hilo endelea kusoma makala hii ili kujua njia za kupata programu za bure kabisa na zenye uhalali asilimia 100%.

Siku hizi kuna njia mbalimbali za kupata programu kwaajili ya kompyuta yako, leo Tanzania Tech tunaenda kuangalia njia halali kabisa ya kukusaidia kupata programu hizo zenye leseni bure kabia bila kutumia gharama yoyote.

  • Kupitia Njia ya Software Informer

Software Informer ni tovuti pamoja na programu ambayo ina kuruhusu kudownload software za bure kabisa kila siku, software hizo hutolewa kwa siku kama sehemu ya ofa na baadae siku inayo fuata software hizo hurudia na kuwa bei yake ya kawaida. Hivyo ni vizuri kudownload software kabla ya muda uliopangwa, unaweza kudowanload software hiyo kwenye kompyuta yako kupitia Hapa.

Advertisement

  • Kupitia Tovuti ya Giveawayoftheday

Tovuti hii ni sawa kidogo na tovuti ya software informer lakini utofauti wake ni kwamba software informer inakupa uwezo wa kudownload programu za bure za mfumo wa window wakati tovuti ya giveawayoftheday inakupa uwezo wa kudownload programu za bure kwa upande wa Android, iOS, Mac pamoja na Windows, unaweza kutembelea tovuti hiyo Hapa.

  • Kuptia Tovuti ya Softpedia

Softpedia ni tovuti inayo julikana sana kwa kutoa sofware za bure na halali kabisa tofauti ya tovuti hii ni kwamba kuna mchanganyiko wa software zinazouzwa na ambazo ni za bure kabisa, kuanza kupata software za bure unaweza kuanzia kudownload Hapa

  • Kuptia Tovuti ya Giveawayclub

Tovuti hii inafanana kabisa na tovuti hiyo hapo juu, lakini utofauti wa tovuti hii ni kuwa inatoa programu na game kwaajili ya kompyuta zenye kutumia mfumo wa uendeshaji wa Windows pekee, Unaweza kupitia tovuti hiyo Hapa.

Na hizo ndio baadhi ya njia ya ambazo unaweza kutumia ili kupata programu za bure na halali kabisa kwaajili ya kompyuta yako, kumbuka programu hizo hutolewa kwa muda maalumu hivyo ni vyema kupitia tovuti hizo ili kuangalia software mpya kila siku.

Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kuwa wa kwanza kupata habari zote za teknolojia, pia unaweza kujiunga nasi kupitia channel yetu ya Youtube ili kapata habari pamoja na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

5 comments
  1. Hakika mnatulimsha uzuri binafsi nawaelewa sana. kazi yenu ni nzuri. Lakini naomba kusaidiwa zaidi maana nimefanikiwa kupakua program ya software iformer nikijaribu kiuifungua naletewa mswali haya what website do you just to visit? what ad did you just click? na coments?…… naomba ofafanuzi hapo.

      1. sawa, hii proglam ya software informer nimeisha idownload ipo kwenye laptop yangu. nikiifungua inafunguka lakini…1. nikienda kweye application ninayotaka kuidownload inafunguka… new tab hunizuia kuendelea kudownload. 2. nikienda kwenye engene search pia inagoma kutype

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use