Jinsi ya Kutengeneza App za Android Bila Kuwa na Ujuzi

Kama unataka kujifunza kutengeneza Application soma hii
App ya Android App ya Android

Ulimwengu kwa sasa umekua sana kiasi kwamba karibia huduma zote unazipata kupitia simu yako ya mkononi, hii imesababisha watoa huduma wote ambao hutoa huduma mtandaoni kulazimika kutengeneza programu (App) kwaajili ya huduma zao, lakini katika kufanya hivyo bado unakutana na changamoto kwani ni lazima kuajiri watu kwaajili ya kufanya hivyo ndio mana leo Tanzania Tech tunakuletea njia hii ya kutengeneza app za android bila kuwa na ujuzi wowote maalum.

Kumbuka hauitaji ujuzi mkubwa kufanya hivi bali unaitajika kuwa na kompyuta yenye uwezo wa kuunganisha internet pamoja na logo na picha mbalimbali za kuweka kwenye programu yako. Ni vyema kuangalia kwanza matumizi kisha ndipo ujue jinsi ya kutengeneza picha na logo za kuweka kwenye App au programu yako, pia ni vizuri kuwa na simu ya android kwaajili ya kutest programu yako kabla ujaamua kuipost kwenye masoko ya Android kama Play Store au Amazoni Store.

Advertisement

Kwa kuanza ni vyema ukajua kuwa ili kutengeneza programu hii ni vyema ukajua unataka kutengeneza programu ya aina gani zifuatazo ni tovuti 10 zitakazo kuwezesha kutengeneza programu mbalimbali kutokana na maitaji yako, lakini sisi tutatumia tovuti ya Adromo kama mfano wetu wa leo.

  1. Mobile Roadie
  2. TheAppBuilder
  3. Appy Pie
  4. AppMachine
  5. BiznessApps
  6. BuzzTouch
  7. Good Barber
  8. Kinetise
  9. Andromo
  10. Como DIY

Kwa kuanza ingia kwenye tovuti ya Andromo kisha tengeneza akaunti kwenye tovuti hiyo, hakikisha unatumia email au barua pepe ambayo utaweza kuingia kwa muda wowote hii ni muhimu sana kwani programu yako itatumwa kwenye barua pepe hiyo baada ya kumaliza kutengeneza programu hiyo, hivyo hakikisha unatumia email sahihi.

Baada ya kujisajili na kuhakiki akaunti yako ingia kwenye akaunti yako kisha utaona mahali palipo andikwa Create New App bofya hapo kisha utaletewa sehemu ya kujaza jina la project hapo hakikisha una andika jina la programu yako kisha bofya Create, baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa ulio andikwa Your App Activities hapo utatakiwa kuweka aina ya vitu ambavyo unataka programu yako ifanye, vitu vyote vinapatikana kwa kubofya sehemu iliyoandikwa Add an Activities ifuatayo ni list ya vitu ambayo utatumia na kazi zake.

  • About – Hapa utaweka ukurasa wa kuhusu programu yako au wewe
  • Audio Player – Hapa utaweza kuweka sehemu ya kucheza muziki
  • Contact – Hapa utaweza kuweka anwani yako
  • Custom Page – Hapa utaweza kuweka ukurasa wowote unaotaka
  • Email – Hapa utaweza kuweka barua pepe
  • Facebook – Hapa utaweza kuweka ukurasa wa facebook
  • Flickr – Hapa utaweza kuonyesha picha kutoka mtandao wa Flick
  • Google Play – Hapa utawea kuonyesha link kwenda kwenye Google Play
  • HTML Archive – Hapa utaweza kuweka ukurasa unaotumia HTML
  • Map – Hapa utaweza kuweka ramani
  • PDF – Hapa utaweza kuweka file la PDF
  • Phone – Hapa utaweza kuweka namba ya simu
  • Photo Gallery – Hapa utaweza kuweka picha mbalimbali
  • Podcast – Hapa utaweza kuweka mfumo wa Podcast
  • RSS Feed – Hapa utaweza kuweka RSS fee ya blog yako
  • SHOUTcast Radio – Hapa utaweza kuweka radio kwenye app yako
  • Twitter – Hapa utaweka ukurasa wao wa Twitter
  • Website – Hapa utaweka tovuti yako
  • YouTube – Hapa utaweka ukurasa wako wa Youtube

Chagua aina ya kitu ambacho unataka programu yako ifanye kisha jaza vitu utakavyo ulizwa kisha endelea mbele kwa kuchagua sehemu ya Style hapo utaweza kuchagua rangi pamoja na aina ya style ambayo unataka programu yako iwe, baada ya hapo endelea mbele kwa kuchagua sehemu ya dashboard hapo utaweza kuchagua aina ya dashbord unayotaka kutumia kwenye app yako kisha save alafu endelea mbele kwa kuchagua Service tumeruka Monetize kwa sababu kwa hii ni app ya bure hivyo hutoweza kuweka matangazao mpaka hapo utakapo lipia kwenye tovuti hiyo kwa maelezo zaidi bofya hapa.

Tukirudi kwenye sehemu ya Service weka namba yako ya Google Analytics ili kujua watu wangapi wanaangalia vitu kwenye programu yako, kisha nenda hatua ya mwisho ambayo ni kutengeneza app yako, sehemu hii inapatikana kwenye Build chagua sehemu hiyo kisha chagua sehemu ya Build My App Hapo subiri kidogo baada ya muda kidogo utapokea barua pepe yenye link ya kudownload App au programu yako.

Ukimaliza hatua zote hizo utakuwa umamaliza kutengeneza programu yako ya kwanza ya Android bila hata kuwa na ujuzi wowote maalum, kama utakuwa unataka kufanya mabadiliko yoyote unaweza kuingia kwenye akaunti yako kisha fuata hatua hizo hapo juu kisha tengeneza tena app yako, kama kuna mahali umekwama usisite kutuandikia hapo chini kwenye maoni na tutakuelekeza.

Soma HapaJifunze jinsi ya kutengeneza App ya Android kwa kutumia Simu yako ya Mkononi.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

140 comments
  1. Habari naitwa Shukuru natokea Tanga ninawazo la kutengeneza app ila nahitaji iwe inaniingizia kipato na nishaandaa maelezo ya app yangu Na kazi inayohusu app kwakua mi ndo wakwanza kufanya hicho kitu kwa hapa kwetu na nahitaji nifanikishe naomba msaada wenu kwani nataka app yangu mtu aweke kujisajili kabla ya matumizi naomba msaada wenu namba zangu ni 0716151915

  2. Nilikua naulizia kwa mfano unataka kutengeneza app kama inst ila inakua na vitu ving ambavyo naviongeza kama servis za hiyo au na kwa mtu anayo fungua account anakua protected je ina kuaje mkuuuuuuuuuh

  3. inawezekana kutumia email ambayo naitumia kwa youtube au ni lazima nitengeneze mpya ? naomba kujua ndugu yangu

Toa majibu kwa Fikiri Ngumbwa Ghairi kujibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use