Programu ya Google Now Launcher Kuondolewa Kwenye Play Store

Google imepanga kuondoa programu ya Google Now Launcher
Google Now Launcher Google Now Launcher

Hivi karibuni hutoweza tena kudownload programu ya Google Now Launcher. Kwa mujibu wa tovuti ya Android Authority programu hiyo itaondolewa kwenye soko la Play Store hapo ifikapo mwishoni mwa mwezi wa tatu.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti hiyo Google itaendelea kuacha programu hiyo ifanye kazi kwa watumiaji wake ambao tayari wamesha install programu hiyo. Kuhusu sababu za kuondoa programu hiyo tovuti hiyo iliandika kuwa, kwa sasa programu zingine zinauwezo wa kuweka sehemu ya Google Now panel ambayo ndio kilikua chanzo cha kuwepo kwa programu hiyo.

Programu hiyo ilizinduliwa rasmi mwaka February 2014, ambapo sasa itakuwa imetimiza miaka mitatu baada ya kuondolewa. Kwa watumiaji wa programu hiyo unaweza kudownload kwa mfumo wa apk na kuwa nayo kama backup kama utahitaji kuitumia baadae.

Advertisement

Ili kupata habari za teknolojia kwa haraka download sasa App ya Tanzania Tech kupitia Play store na tuna ahidi kukupa habari zote za teknolojia kwa haraka kila siku. Pia unaweza kujiunga na channel ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili kupata habari na maujanja mbalimbali kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use