in

Kutana na Gita Roboti ya Kukusaidia Kubeba Mizigo Mahali Popote

Roboti mpya ya kukusadia kubeba mizigo yako popote uendapo

Roboti ya Gita

Roboti zinaonekana kuja kwa kasi sana kudhibitisha hilo hivi karibuni kampuni ya Piaggio yenye makao makuu yake huko Pontedera, Italy imezindua roboti mpya ya kukusaidia kubeba mizigo inayoitwa Gita.

Roboti hiyo ya Gita imetengenezwa kwa kutumia kamera maalum pamoja na mkanda ambao mtumiaji uvaa kiunoni na roboti hiyo ufuata mkanda huo uku ukiwa imebeba mizigo yako, roboti hiyo inatumia sehemu zote kama vile ilivyo pikipiki ndogo hivyo ina uwezo wa kutembea kwa kasi ya speed ya mile 22 kwa lisaa limoja ikiwa na uwezo wa kukufuata hata kama uko kwenye baskeli.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Vilevile Gita inauwezo wa wakutembea yenyewe baada ya kujua inapokwenda kwani roboti hiyo imetengenezwa na kuekewa ramani maalum ambayo hutumiwa na roboti hiyo baada ya kuionyesha njia kwa mara ya kwanza. Taarifa zote za mahali pa kwenda huifadhiwa kwenye ramani hiyo na baadae kutumiwa na roboti hiyo kujua unapotaka ipeleke mzigo wako.

Roboti hiyo ya Gita inategemewa kutoka mwezi huu na bado haijajulikana rasmi kuwa itauzwa kwa bei gani, watu wengi mtandaoni wanaonekana kupenda roboti hiyo na kusema kuwa itakuwa msaada mkubwa kwa watu wengi wanaotaka kubeba mizigo mingi wanapo kwenda mahali.

Kutana na Gita Roboti ya Kukusaidia Kubeba Mizigo Mahali Popote
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.