in

Dell Kuleta Toleo Jipya la Laptop ya XPS 13 Lenye Uwezo wa 2-in-1

Toleo jipya la laptop kutoka kampuni ya Dell XPS 13 sasa yaja na 2-in-1

Toleo la laptop kutoka kampuni ya Dell, XPS 13 ni moja kati ya laptop bora sana za mwaka 2016. Laptop hii imekua ni pendekezo la watu wengi sana kutokana na muundo pamoja na uwezo wa laptop hii, Pengine hii ndio sababu mwaka huu 2017 kampuni ya Dell imetangaza kuwa itarudisha tena sokoni toleo hilo ambalo sasa laptop hiyo itakuwa na uwezo wa 2 in 1.

Laptop hiyo ambayo sasa itakuwa na uwezo wa laptop pamoja na tablet itakuja ikiwa na maboreshwa pamoja na kuongezewa uwezo zaidi. Laptop hiyo imeonekana kwanza kwenye tovuti ya dell ambapo laptop hiyo inategemewa kutoka kupitia kwenye mkutano wa CES EXPO utakaofanyika huko Las Vegas mwezi February mwaka huu 2017.

Kwa habari zaidi kuhusu laptop hii endelea kutembea Tanzania Tech au unaweza kupata habari zote kwa haraka zaidi kupitia App yetu ya Android ya Tanzania Tech ambayo inapatikana kupitia Play Store.

Kampuni ya Xiaomi Yazindua Laptop Mpya za Mi NoteBook 14
Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.