in

Nokia Yazindua Simu Mpya ya Nokia 6 yenye Kutumia Android

Hii ndio simu mpya ya Nokia 6 yenye kutumia mfumo wa uendeshaji wa Android

Nokia 6

Kwa muda sasa kumekua na habari mbalimbali kuhusu simu mpya za Nokia ambazo sasa zitakuwa zikitumia android, katika kudhibitisha habari hizo hapo jana kampuni ya nokia ilitoa simu yake ya Nokia 6 ya kwanza ambayo sasa itakua ikitumia mfumo wa uendeshaji wa Android.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Simu hiyo ina sifa za RAM ya GB 4, ukubwa wa memory ya ndani GB 64 ambao unaweza kuongeza kwa kutumia Memory Card, bila kusahau simu hii sasa itakuwa inatumia Android 7.0 Nougat. Vile vile Nokia 6 inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 8 pamoja na kamera ya nyuma ya Megapixel 16, pia simu hiyo mpya inakuja na teknolojia mpya za phase-detect AF, pamoja na Fingerprint.

Kwa bahati mbaya Nokia haitegemei kutoa simu hii ya Nokia 6 nje ye mipaka ya china hivyo kama wewe ni mpenzi wa Nokia ni vizuri ukiendelea kusubiria simu nyingine kutoka Nokia sababu nokia haijaishia hapo kwani inategemea kutoa simu nyingine nyingi mwaka huu zenye kutumia Android.

Kupata habari zote za teknolojia pindi zitakapo toka endelea kutembelea Tanzania tech au unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play Store.

Nokia Yazindua Simu Mpya ya Nokia 6 yenye Kutumia Android
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.