Kwa muda sasa kumekua na habari mbalimbali kuhusu simu mpya za Nokia ambazo sasa zitakuwa zikitumia android, katika kudhibitisha habari hizo hapo jana kampuni ya nokia ilitoa simu yake ya Nokia 6 ya kwanza ambayo sasa itakua ikitumia mfumo wa uendeshaji wa Android.
Simu hiyo ina sifa za RAM ya GB 4, ukubwa wa memory ya ndani GB 64 ambao unaweza kuongeza kwa kutumia Memory Card, bila kusahau simu hii sasa itakuwa inatumia Android 7.0 Nougat. Vile vile Nokia 6 inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 8 pamoja na kamera ya nyuma ya Megapixel 16, pia simu hiyo mpya inakuja na teknolojia mpya za phase-detect AF, pamoja na Fingerprint.
Kwa bahati mbaya Nokia haitegemei kutoa simu hii ya Nokia 6 nje ye mipaka ya china hivyo kama wewe ni mpenzi wa Nokia ni vizuri ukiendelea kusubiria simu nyingine kutoka Nokia sababu nokia haijaishia hapo kwani inategemea kutoa simu nyingine nyingi mwaka huu zenye kutumia Android.
Kupata habari zote za teknolojia pindi zitakapo toka endelea kutembelea Tanzania tech au unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play Store.