in

Samsung Kutoa Sababu Halisi ya Note 7 Kulipuka Mwezi Huu

Baada ya uchunguzi sasa Samsung inatarajia kutoa sababu rasmi za Note 7 kulipuka

Samsung Kutoa Sababu Halisi ya Note 7 Kulipuka Mwezi Huu

Mwaka 2016 ni mwaka ambao hauta saulika kwenye historia ya simu za mkononi za samsung pamoja na kampuni hiyo kwa ujumla, Historia hiyo ilitokana na kampuni hiyo kupata hasara ya mamilioni ya pesa baada ya kuanza kulipuka kwa simu za Samsung Galaxy Note 7 siku chache tu baada ya simu hizo kuingia sokoni.

Hivi karibuni kampuni hiyo ya samsung imetangaza rasmi kuwa mwezi huu itatoa sababu halisi ya simu hizo kulipuka baada ya sababu ya ubovu wa battery kuonekana sio chanzo halisi cha simu hizo kulipuka. Habari kutoka kwenye tovuti ya Korea Herald zinasema kuwa samsung imeshirikiana na baadhi ya kampuni kufanya uchunguzi juu ya nini kilisababisha tatizo la simu hiyo kulipuka.

Kampuni hizo ni pamoja na US-based Underwriter Laboratories pamoja na makampuni ya Usalama ya Sayansi (Leading Safety Science Company) yote ya nchini marekani. Bado kwa sasa haijajulikana tarehe rasmi ambayo samsung itatoa taarifa hizo ili kupata taarifa hiyo pindi itakapo toka endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Video : Ugumu na Ubora wa Simu Mpya ya iPhone 12 Pro

UPDATE

Samsung imetangaza leo kuwa siku ya jumapili ya tarehe 22 itatoa ripoti ya chanzo cha kulipuka kwa simu mpya ya Samsung Galaxy Note 7. Kaa Tayari kujua chanzo cha kulipuka kwa Note 7 kupitia Tanzania Tech kwani tutakua tukionyesha matangazo hayo live. Unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari hizo na nyingine nyingi pindi zitakapo toka.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.