Najua kuna wakati unatamani ungekuwa na uwezo wa kuosha smartphone yako, pengine ni kwa sababu unataka kuondoa uchafu fulani au unataka tu! simu yako iwe kwenye hali ya usafi zaidi ya inavyokuwa kawaida. Kuwezesha hilo kampuni ya nchini Japan Kyocera Corporation leo imetengaza na kuzindua rasmi smartphone yenye uwezo wa kuoshwa na maji na sabuni.
Simu hiyo iliyotengenezwa kwa teknolojia maalum ya kuzuia sabuni ndio smartphone pekee duniani yenye uwezo wa kuoshwa kwa sabuni na maji ya moto. Simu hii inatarajiwa kutoka mwezi March huko nchini Japan na inatagemewa kutoka na rangi tatu za Pale Pink, Clear White and Light Blue.
Vile vile simu hiyo inauwezo wa kutumiaka hata kama kioo chake kimeloa kabisa na maji huku ikikupa uwezo wa kupokea simu hiyo pale inapo-pigwa bila kuigusa (kwa hutumia sensor maalum). Sifa zingine za simu hiyo ni kama vile, Internal memory: 16GB ROM / 2GB RAM, External memory: microSDXC™ (up to 200GB), 4G LTE / WiMAX2+, Battery 3,000mAh (provisional) pamoja na mfumo wa undeshaji wa Android 7.0 (Nougat).
Bado haijajulikana kama simu hiyo itasambaa kote duniani bali kwa sasa simu hiyo inategemewa kupatikana kwa nchi ya Japan pakee.