Programu Bora Kwaajili ya Kuangalia Filamu Kwenye Simu

Kama unataka kuangalia filamu kwenye simu, hizi ndio programu bora
Filamu kwenye Simu Filamu kwenye Simu

Kuna wakati unajikuta unalazimika kuangalia filamu (Movies) kwenye simu yako ya mkononi (smartphone), tatizo ni kwamba ni ngumu sana kupata programu au sehemu itayokusaidia kupata movie au filamu bora na mpya kwa haraka. Kukusaidia kwenye hili Tanzania Tech tunakuletea programu bora za kuangali filamu mpya kwenye simu yako ya Android.

  • Crackle – Free TV & Movies
Crackle
Price: Free

Hii ni programu bora sana kwa kuangalia filamu kwenye simu yako, programu hii ni bure kabisa na inasifika na watu wengi ikiwa na download zaidi ya 10,000,000.

  • Hotstar TV Movies Live Cricket
Hotstar
Price: To be announced

Programu hii ni moja kati ya programu bora ya kuangalia filamu kutoka india, kama wewe ni mpenzi wa filamu kutoka india basi ni vyema kuijaribu programu hii yenye download zaidi ya 50,000,000.

Advertisement

  • Viewster – Movies, TV & Anime

Hii ni programu nyngine bora ya kuangalia filamu kwenye simu ikiwa inakupa uwezo wa kuangalia filamu mbalimbali ikiwa ni pamoja na filamu za katuni, filamu za kutisha na makala mbalimbali, programu hii inaonekana kuvutiwa na watu zaidi ya 5,000,000 walio download programu hiyo.

  • JustWatch – Movies & TV Shows

JustWatch ni programu nyingine inayokupa uwezo wa kuangalia filamu kwenye simu yako, programu hii inaongoza kwa kuwa na mkusanyiko mkubwa wa filamu mpya mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi. Programu hii inaonekana kupakuliwa zaidi ya mara 1,000,000.

  • Flipps – Movies, Music & News

Hii ni programu nyingine inayokuwezesha kuangalia live filamu moja kwa moja kwenye simu yako, programu hii ni maarufu kwa kuwa na filame zenye format ya HD pekee. Kama wewe ni mpenzi wa filamu zenye teknolojia ya HD basi ni vizuri kujaribu programu hii kwani tayari watu zaidi ya 1,000,000 wanatumia programu hii bora ya filamu.

  • Tubi TV – Free Movies & TV

Tubi TV ni programu inayokupa uwezo wa kuangalia filamu mbalimbali maarufu, programu hii inakupa uwezo wa kuangalia filamu baadhi kutoka kwenye Netflix hivyo kama wewe ni mpenzi wa filamu kutoka Netflix jaribu programu hii inayotumiwa na watu zaidi ya 10,000,000.

  • Netflix
Netflix
Price: Free

Hii ni programu ni maarufu na ambayo watu wengi wanaijua kwa kuptia programu hii utaweza kuangalia filamu mpya kabisa kutoka nje na ndani ya marekani, programu hii inalipiwa na tayari watu zaidi ya 100,000,000.

Na hizo ndio baadhi ya programu za kupata filamu pamoja na Tamthilia mpya kwenye simu yako ya mkononi ya android. Kama unahisi kuna programu ilikua inatakiwa kwenye list hii tumbie kupitia maoni hapo chini.

Kuendelea kupata habari zaidi za teknolojia kwa haraka Download App yetu ya Tanzania Tech inayopatikana kupitia Play Store au unaweza kujiunga na channel yetu ya Yutube ili kupata habari kwa njia ya video kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use