Hii Ndio Picha Iliyovuja ya Simu Mpya ya Samsung Galaxy S8

Picha iliyovuja ya Samsung Galaxy S8 ikiwa na rangi ya Gold

Picha za tetesi za simu mpya ya Samsung Galaxy S8 zimekua nyingi sana, ukitegemea simu hiyo inatarajiwa kutoka mwezi February basi tetesi nazo zimezidi kuwa nyingi sana. Lakini leo uko nchini china kupitia tovuti ya Weibo service zimevuja picha ambazo zinasemekana ndio picha halisi za simu hiyo mpya kutoka kampuni ya Samsung.

Picha kutoka Weibo

Picha hii inasemekana ndio picha halisi ya simu mpya ya Samsung Galaxy S8 lakini bado hakuna uhakika kama simu hiyo ndivyo itakavyokuwa, lakini kwa mtazamo tu uwezekano wa simu hii kuwa ndio samsung galaxy s8 ni mkubwa sana.

Ngoja tuone kwenye uzinduzi wa simu hiyo utakaofanyika mapema mwezi February kwenye mkutano wa CES wa Mwaka 2017, Kujua zaidi kuhusu simu hii na kuangalia uzinduzi wa simu hii endelea kutembelea Tanzania Tech pamoja na kipengele cha CES 2017 kila siku.

Tanzania Tech

Follow us @Tanzania Tech

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Akaunti yako ya Google inatumika kutoa Maoni (Vigezo na Masharti Kuzingatiwa)

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.