Teknolojia Mpya ya Magari Kwenye Mkutano wa CES 2017

Magari nayo pia yalikua kwenye mkutano wa CES wa mwaka 2017
Magari CES Magari CES

Teknolojia ya magari imeendelea kukua kila siku, ili kukuletea yote unayotakiwa kujifunza na kujua kuhusu magari Tanzania tech itakuletea kipengele maalum cha magari ambacho hapo tutakua tukijifunza wote kuhusu teknolojia zote mpya za magari kwa ujumla.

Tukirudi kwenye mkutano wa CES wa mwaka huu, magari nayo yalikwepo kwenye mkutano huo ambao sasa umeingia kwenye siku ya nne. Ifuatayo ndio list ya teknolojia bora za magari zilizokua kwenye mkutano huo.

Advertisement

FF 91

FF 91 ni aina ya gari la umeme ambalo linategenezwa na kampuni ya Faraday Future kampuuni ambayo pia mwaka jana ilikuja na magari ambayo ni bora na ya kisasa kabisa.

Chrysler Portal

Hii ni gari nyingne tena ambayo imekuja na teknolojia mpya na ya kisasa kabisa, kujua zaidi kuhusu gari hili endelea kutembelea tanzania tech kila siku.

Delphi’s autonomous Audi

Delphi’s autonomous Audi ni gari la kisasa lenye teknolojia ya kujiendesha lenyewe, gari hili limeshinda tuzo za moja kati ya gari bora linalojiendesha lenyewe, kujua zaidi kuhusu gari hili endelea kutembelea Tanzania tech.

BMW i Inside Future

Hilo ni gari jipya kutoka kwa kampuni maarufu ya BMW, magari ya aina hii yanategemewa kutoka kwa miaka ya baadae sana. lakini kama unataka kujua zaidi endelea kutembelea Tanzania tech.

Toyota’s Concept-i

Toyota’s Concept-i ni gari linalotegemewa kuja kwenye miaka ya karibuni, gari hili linatumia kompyuta kwenye karibia kila kifaa chake ili kujua zaidi endelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Hyundai Mobility Vision

Hyundai pia haikua nyuma kwenye mkutano wa mwaka huu, kampuni hiyo ilionyesha matarajio yake ya magari yatakayokuja kwenye miaka ya karibuni.

Ioniq Scooter

Ioniq Scooter ni mfano wa pikipiki ndogo ambayo unaweza hata kuibeba kwenye begi lako hii itakusaidia kama wewe unataka kukatisha kwenye mitaa mbalimbali kwa haraka.

Na hii ndio list ya teknolojia mpya za magari ambazo zinakuja au zinategemewa kuja kwenye miaka ya karibuni. Kama unataka kujua zaidi kuhusu magari mabalimbali endelea kutembelea Tanzania Tech kwani tunaandaa kipengele cha magari ili kukusaidia kujua kuhusu magari pamoja na teknoloji yake kwa ujumla.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use