Kampuni ya Yahoo Kuwa “Altaba” Kama Ikinunuliwa na Verizon

Kampuni ya yahoo kubadilishwa jina na kuwa Altaba kama ikinunuliwa na Verizon
Altaba Altaba

Bado mpaka sasa haijajulikana kama kampuni ya Verizoni itakubali kununua kampuni ya yahoo kwa dollar za marekani  $4.8 billion, lakini hivi karibuni wakati mapatano yakiendelea Verizon imetangaza kuwa kama ikinunua kampuni hiyo basi itabadilisha jina la kampuni hiyo kuwa Altaba. Kwa miezi sasa kampuni ya yahoo imekua ikifanya makubadilano mbalimbali pamoja na kupitishwa chini ya wakaguzi mbalimbali ili kukamilisha ununuzi wa kampuni hiyo  ambao utafanywa na kampuni ya Verizon.

Kwa muda wote huo kampuni ya yahoo imekua ikiita sehemu ya kampuni yake iliyobaki “RemainCo” na sehemu hii ya kampuni iliyo baki ndio itakayoitwa “altaba” endapo kampuni ya Verizoni itanunua sehemu hiyo, Wataalamu kupitia tovuti ya The Wall Street Journal wemeeleza jinsi jina hilo lilivyopatikana. Watalamu hao wamesema kuwa “RemainCo” au kiasi cha mali kilichobaki kwenye kampuni ya yahoo kinahusiana na kampuni ya Alibaba Group Holding Ltd pamoja na Yahoo Japan ambapo mchanganyiko wa majina ya ‘alternate’ and ‘Alibaba, ndio wenye kuleta jina la Altaba, walisema wataalamu kutoka kwenye tovuti hiyo.

Hata hivyo ununuaji wa kampuni ya yahoo utasababisha mabadiliko mengi zaidi ya jina hilo, kwa mujibu wa regulatory document utawala wa sasa wa kampuni hiyo ni lazima ubadilishwe na zaidi ya viongozi 11 wata takiwa kusimamishwa kazi kutoka kwenye kampuni hiyo. Mpaka sasa bado haijajulikana kama kampuni ya Verizon itanunua mtandao huo.

Advertisement

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use