Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuzuia Mtu Kuhack Akaunti Yako ya Mtandao wa Instagram

Fuata hatua hizi ili kuzuia mtu asiweze kuhack akaunti yako ya Instagram
kuhack instagram kuhack instagram

Instagram imekua ni sehemu muhimu katika swala zima la kutafuta masoko, karibia kila mtanzania mwenye smartphone hivi sasa ni lazima anatumia mtandao huo. Kutokana na umuhimu wake watu hutumia nguvu kubwa pamoja na pesa kupata follower wengi ilimradi mtu aweze kufikia lengo lake la kutangaza biashara yake kwa namna mpya na yakisasa kabisa.

Umuhimu huu ndio unao sababshwa watu kufikiria kuhack akaunti za watu flani ili kujipatia followers pamoja na kutangaza biashara zao. Katika kuhakikisha hali hiyo haitokei leo Tanzania Tech tunakuletea njia rahisi za kuzuia watu au mtu asiweze kabisa kuhack akaunti yako ya Instagram, moja kwa moja bila kupoteza muda twende tukangalie njia hizo.

Advertisement

Njia za Kawaida

  • Hakikisha unatumia password ngumu yenye mchanganyiko wa alama, namba pamoja na herufi, pia ni vyema kutumia alama hizi (! na &) kwenye password yako kwani zinaongeza ugumu pamoja na kudumu kwa password yako.
  • Badilisha Nywila (Password) yako kila mara hasa pale unapoona meseji kutoka Instagramu ikitaka ufanye hivyo, Hii ni muhimu sana kwani instagram hupendelea kutuma meseji hizo pale wanapoona akaunti yako ina dalili za ku-hackiwa.
  • Hakikisha (email) barua pepe yako iko salama kwani mtu yoyote mwenye uwezo wa kuingia kwenye email yako basi pia mtu huyo anauwezo wa kuhack akaunti yako ya instagram.
  • Hakikisha una Log out pale unapotumia simu au kompyuta ya mtu kuangalia akaounti yako ya Instagram.

Njia za Muhimu 

  • Hakikisha unaweka namba yako ya simu kwenye akaunti yako kwani mara nyingi namba hii inaweza kukusaidia kurudisha akaunti yako iliyo hackiwa.
  • Hakikisha hautumii password sawa na ya email au mahali pengine popote, kifupi hakikisha una tengeneza password kwaajili ya instagram pekee zizifanane na password unazotumia popte.
  • Hakikisha unawasha sehemu maalum ya Two-Factor Authentication sehemu hii inakusaidia kutumia password maalum pale unapotaka kuingia kwenye akaunti yako kwenye kifaa tofauti na simu yako. Ili kuwasha sehemu hii nenda kwenye profile yako kisha bofya settings kisha utaona sehemu iliyoandikwa “Two-Factor Authentication” bofya hapo kisha seti sehemu hiyo kwa kutumia simu yako.
  • Hakikisha unazuia matumizi ya akaunti yako ya instagram kwenye programu zingine, kwa mfano unakuta kuna mahali umeambiwa unaweza ku-login kwa kutumia akaunti yako ya instagram. ili kulinda akaunti yako usipendelee kufanya hivyo badala yake tumia njia za kawaida za kujisajili kwenye akaunti mbalimbali mtandaoni.

Hitimisho

Ongezeko la matumizi ya mtandao ndio yanayosababisha mtu aweze kuhack akaunti yako, kwani hacker hutumia akaunti zako zingine kuweza kujua password zako hivyo ni jambo la muhimu kutokutumia password zinazofanana na akaunti zingine zozote mtandaoni.

Kama akaunti yako imekuwa hacked na unatafuta namna ya kuirudisha unaweza kuwasiliana na Instagram kwa kutumia fomu hii hapa. Pia kumbuka kuhifadhi password zako sehemu salama ili usiweze kusahau.

6 comments
  1. Naitwa veronica kiwuyo gmail yangu kuna mtu anaitumia anaitwa happy laulencin.naomba msaada wenu

    1. Habari, Kana mambo mengi ya kuangalia hapa kabla ya yote. je una uwezo wa kuingia kwenye email yako kwa sasa..?

  2. Kuna m2 kaniuzia account ya Instagram nimebadili email namba jina lakin Bado anaingia na anabadili nifanyeje

      1. Sehem zote hizo niliwasha na akaweza kuingia nilichokifanya now nimewasha hiyo nikaandika namba yangu nikabadil email pia nikazima hiyo authentication sijui itakuwa sawa

  3. Habar kaka,Mimi nimeibiwa account yangu ya biashara,nafanyaje ili kuirudisha na password nimeishau nifanyeje?naomba msaada.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use