Hatimaye Samsung imetangaza chanzo cha kulipuka kwa Samsung Galaxy Note 7, simu ambayo ililazimika kutolewa sokoni hapo mwaka jana baada ya watu kuanza kutoa taarifa mbalimbali za kulipuka kwa battery ya simu hiyo.
Katika ripoti yake samsung imetangaza kuwa kulikua na matatizo kwenye battery zote za simu hiyo, yaani ile iliyotoka na simu na ile iliyobadilishwa baada ya simu hizo kuanza kulipuka. Samsung ilisema kuwa battery ya kwanza ili kua na matatizo kwenye kona ya kulia juu ya battery hiyo ambayo ilikua ikisababisha shoti saketi na kusababisha simu hiyo kushika moto. Battery ya pili nayo ilikua na matatizo katika utengenezaji kwa kuwa na matatizo yaliyosababishwa wakati wa uunganishaji wa makava ya battery hiyo (welding defect).
Kampuni hiyo imefanya uchunguzi huo kwa kutumia wafanyakazi wake zaidi ya 700 na simu zaidi ya 200,000 pamoja na battery zaidi ya 30,000. Vilevile Samsung ilifanya kazi na kampuni za nje tatu tofauti UL, Exponent pamoja na TUV Rheinland, ambapo kampuni zote tatu zilipata majibu sawa sawa na majibu yaliopatikana na kampuni ya Samsung.
Katika michoro hii liyotolewa na Kampuni ya Samsung inaelezea kwa undani matatizo hayo yaliotokea kwenye simu hiyo ya Samsung Galaxy Note 7.
Mkutano huo wa Samsung ulikua ukionyeshwa live, bado tunafanya jitihada za kpata video ya mkutano huo endelea kutembelea makala hii ili kuweza kukupa taarifa zaidi jinsi ilivyokuwa kwenye mkutano huo wa Samsung.
Kwa habari zaidi unaweza kudownload app ya Tanzania tech kupitia Play Store ili kupata muendelezo wa habari hii kwa haraka zaidi. Pia kama unataka kujifunza na kupata habari za mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video unaweza kuangali Channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube.