Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Bidhaa Bora Mpaka Sasa Kwenye Mkutano wa CES 2017

Hizi ndio baadhi ya bidhaa ambazo zimeshika chati kwenye mkutano wa CES 2017
teknolojia bora CES 2017 teknolojia bora CES 2017

Mkutano mkubwa wa teknolojia duniani CES bado unaendelea na sasa ni siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika huko Las Vegas, Nevada. Kwa siku ya jana tuliona baadhi ya makampuni kama vile Samsung, LG, Sony na makampuni mengine yakionyesha bidhaa zao zinazokuja ndani ya mwaka huu wa 2017.

Leo siku ya pili makampuni mengine yameonyesha bidhaa zao kwenye mkutano huo na hizi ndio kati ya bidhaa ambazo ni maarufu mpaka sasa kwenye mkutano huo wa Consumer Electronics Show (CES) wa mwaka huu wa 2017.

Advertisement

Samsung Chromebook Plus

Kwenye mkutano huu kuna bidhaa nyingi ambazo ni bora sana na ambazo zinatumia teknolojia za kisasa, moja kati ya bidhaa hzo ni Samsung Chromebook Plus hii ni aina ya kompyuta mpakato au (Laptop) ambayo inatumia Android kama mfumo wa uendeshaji, kizuri kuhusu laptop hii ni kuwa sasa unauwezo wa kudownload App moja kwa moja kutoka play store.

Kwa uwezo wake wa kioo cha inch 12.3 touchscreen display, Quad HD resolution pamoja na uwezo wa kutumia S Pen laptop hii ni moja kati ya laptop ambayo ni bora kuwa nayo mwaka 2017. Laptop hii inaendeshwa na processor ya 2.0GHz hexa-core processor ambayo inaipa nguvu ya kutosha kucheza game pamoja na kufanya kazi zingine nzito kiasi kwenye laptop hii.

LG Signature OLED TV W7

Unapokuja kwenye swala zima la teknolojia ya TV kwa mwaka huu lazima utazungumzia TV hii ya LG Signature OLED TV W7, kwani hii ndio kati ya TV nyembamba kuliko zote. TV hii ina unene wa mm 2.59 nyembamba kuliko hata simu ya iPhone 7.

TV hii ya kisasa inatambulisha teknolojia mpya na bora za 4K Ultra HD resolution pamoja na HDR kifupi ni kwamba, LG Signature OLED TV W7 ni moja kati ya TV ambazo kwa hakika inatambulisha ulimwengu mpya wa teknolojia ya TV kwa miaka inayokuja.

AirBar

AirBar ni kifaa kipya ambacho kinawezesha kompyuta ya Apple kuwa na Touchsreen, unachotakiwa kufanya ni kuchomeka kifaa chako kwenye kompyuta na hapohapo utaweza kuanza kutumia kompyuta yako kwa kutumia Touchscreen.

Kifaa hichi kinapatikana kwenye mfumo wa kompyuta za Apple pekee na bado haijajulikana kama kifaa hicho kitakuja kwenye mfumo wa kompyuta za PC au Windows.

Sleep Number 360 Smart Bed

Linapokuja swala la teknolojia hapa ndipo tunapo shagazwa na kujiuliza miaka kumi baada ya mwaka huu tutakua wapi..?, kujibu swali hili ni lazima uangalie teknolojia hii mpya ya kitanda kinachoitwa Sleep Number 360 Smart Bed kitanda hichi kinauwezo wa kujifunza kuhusu kulala kwa ili kiweze kukupa usingizi unaotakiwa.

Kitanda hichi kinauwezo wa kujua ni muda gani mzuri kwako kulala na kiasi cha joto au baridi inayotakiwa ili uweze kulala, zaidi Sleep Number 360 Smart Bed kinauwezo wa kukupa bairidi au joto kwa pande mbili tofauti, haijaishia hapo kitanda hichi ni zaidi ya kitanda kujua hayo angalia video hapo juu. Bila shaka mpaka sasa unaanza kujua teknolojia itakuwa wapi miaka kumi ijayo kama bado huniamini endelea kusoma makala hii.

Sevenhugs

Sevenhugs ni aina ya remote ambayo inauwezo wa kuendesha karibia kila kitu kwenye nyumba yako, remote hii inakuwezesha kuacha kuwa na remote nyingi kwa kila kifaa utakachonunua, Bali sasa utakuwa na remote moja tu kwaajili ya kila kitu kwenye nyumba yako kuanzia taa, TV, mpaka redio na vitu vingine vinavyoitaji remote.

Whirlpool Zera Food Recycler

Whirlpool Zera Food Recycler ni chombo cha takataka kinachoweza kubadilisha takataka za chakula kuwa mbolea ndani ya masaa 24, hii ni moja kati ya teknolojia mbayo ukweli kabisa inahitajika kwenye nyumba na mahoteli hapa Tanzania. Kwa kutuimia teknolojia hii unaweza hata kuazisha biashara ya mbolea kwa kutokana na taka za chakula chako kutoka nyumbani.

Bado zipo teknolojia nyingi sana ambazo tutaendelea kukuletea kadri mkutano huo jinsi utakavyoendelea. Kumbuka kutembelea kipengele maalumu cha CES 2017 ili kujua yote yanayojiri kwenye mkutano huo wa teknolojia duniani.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use