Viatu Hivi Vinauwezo wa Kubadilika na Kuwa na Muonekano Unaotaka

Viatu hivi vya kisasa vinauwezo wa kubadilika staili yake na kuwa staili unayotaka
Viatu Viatu

Mwaka 2017 umeanza na teknolojia nayo bado inaendele kusonga mbele na kukua kila siku, leo huko nchini marekani wataalamu wa teknolojia wametengeneza viatu visivyo chakaa. Kutoku chakaa kwa viatu hivyo kuna sababishwa na uwezo wa viatu hivyo kubadilika na kuwa jinsi unavyotaka.

Viatu hivyo vya aina ya Snekers Vixole v10 vinaendeshwa kwa kutumia simu ya mkononi (smartphone) kupitia proramu maalum ya Android na iOS. Kuwezesha teknolojia hiyo viatu hivyo vimetengeneza na kioo maalumu cha LED ambacho kiko nyuma ya kiatu hicho kikiwa ndio kinauwezo wa kubadilika na kukipa kiatu hicho muonekano tofauti kila mara.

https://www.youtube.com/watch?v=wQU1u6ud-Wg

Advertisement

Mmiliki wa viatu hivyo atakuwa na uwezo wa kuchangua aina ya rangi, maua au wallpaper ambayo ndio itakuwa ikisaidia kiatu chako kupata muoneknano mpya kwa urahisi kabisa kwa kutumia simu yake ya mkononi. Vile vile viatu hivyo vinatumia battery maalum ambayo ina dumu zaidi ya masaa nane ikiwa imejaa mpaka asilimia 100, kwa sasa viatu hivyo vitapatika kwa dollar za marekani $160 viatu hivyo vinategemewa kuingia sokoni mwezi June 2017.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use