Angola Kuongoza kwa Kuuza iPhone Bei Rahisi Kuliko Nchi Zote

Utafiti unaonyesha kuwa iphone inauzwa bei rahisi nchini angola kuliko nchi zote
iphone iphone

Wafanya biashara wengi wa simu hapa Africa wamekua wakisafiri kwenda nchi za china, marekani pamoja na nchi zingine za mataifa ya ulaya ili kununua simu hizo kwa bei nafuu na baadae kuja kuuza simu hizo kwa faida kwenye nchi mbalimbali za Africa. Pengine utafiti huu unaweza kubadilisha jinsi wafanya biashara hawa wanavyo fanya biashara hiyo ya simu.

Wote tunajua simu za aina ya iPhone zina sifa nyingi sana na moja kati ya sifa hizo ni simu hiyo kuuzwa kwa bei ghali sana, pengine kama wewe unatoka nchini Angola lazima uta bisha kuhusu jambo hilo kwani kwa mujibu wa utafiti wa mwaka jana (2016) kutoka Technology Price Index unaonyesha kuwa nchi ya Angola ndio nchi pekee inayongoza kwa kuuza simu hizo kwa bei ya chini kuliko nchi zingine zote duniani.

Nchini Angola iphone inauzwa kwa kiasi cha dollar za marekani $400 sawa na shilingi za tanzania Tsh 900,000 ikiwa na tofauti ya dollar za marekani $200 kama utanunua simu hiyo nchini marekani. Ifuatayo ni orodha ya nchi zinazo uza simu hiyo kwa bei nafuu ikianza nchi ya Angola.

Advertisement

Simu za Bei rahisi
Provided by Quartz

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya Linio kupungua kwa bei hiyo kunachangiwa na kupungua kwa kodi mbalimbali nchini humo ikiwa ni pamoja na kodi za usafirishaji pamoja na kodi zingine za uingizaj wa bidhaa hizo.

Bila shaka wafanya biashara sasa wanaweza kubadilisha muonekano wa biashara zao za simu na kuanza kwenda nchini Angola kununua simu hizo za iphone kwa bei nafuu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use