Kampuni maarufu ya teknolojia ya Western Digital, inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya data kama vile hard disk, flash drive na vifaa vingine kama hivyo hivi karibuni imetangaza sasa inafanya majaribio ya kuingiza sokoni hard disk zenye ukubwa wa Terabit 14 (TB14).
Ikiwa ni moja kati ya kampuni zilizojiwekea rekodi kwa kuleta hard disk hiyo ya TB 14, Western Digital kwa sasa inasambaza hard disk hizo kwa wateja maalumu kwaajili ya kufanyiwa majaribio ili ziweze kuingia sokoni mapema mwaka 2017.
Western Digital imeongeza ufanisi zaidi katika utengenezaji bidhaa bora za teknolojia baada ya kampuni hiyo kununua kampuni ya SanDisk, kampuni ambayo mwaka huu ilitoa memory card kubwa kuliko zote ya 1TB. Hata hivyo kampuni ya Western Digital bado haijatangaza hard disk hiyo itapatika kwa bei gani. Hard disk hii inategemea kutoka kwa matoleo mawili ambayo ni ya 14TB na 12TB.
Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.