Kampuni ya teknolojia ya Microsoft, leo imetangaza kuwa sasa iko tayari kuleta uwezo wa kompyuta kwenye Simu za mkononi. Kampuni hiyo imesema kuwa kwa sasa imefanikiwa kuwezesha toleo zima la Windows 10 kufanya kazi vizuri kabisa kwenye simu za mkononi zenye kutumia processor za ARM chipsets.
Katika video hii iliyotokewa na kampuni hiyo leo imeonyesha, Windows 10 ikifanya kazi vizuri kabisa kwenye kifaa kinachotumia Qualcomm Snapdragon 820 processor, ikiwa na uwezo wa kufanya kazi kwa programu mbalimbali kama vile Adobe Photoshop pamoja na Microsoft Office.
Hata hivyo uwezekano huu unaweza kuanza na laptop zenye processor za ARM-based laptops kutoka kampuni ya microsoft ambazo awali zilikua zikitumia windows 10 kwaajili ya simu sasa zitaweza kutumia toleo zima la Windows 10 pamoja na programu zake zote kama ilivyo kwenye kompyuta ya kawaida.
Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.