Facebook hapo juzi ilitangaza kuwa kwa sasa ipo tayari kuachia game nyingine mpya ya PAC-MAN ambayo watumiaji wa Facebook Messenger wataweza kucheza game hiyo moja kwa moja kupitia programu hiyo yaani Facebook Messenger.
Game hiyo mpya inakuja moja kwa moja na uwezo wa kucheza game hiyo na nyingine nyingi kwenye programu hiyo kwa kubofya kitufe maalum, mtumiaji wa Facebook Messenger ataweza kucheza game hizo na marafiki na baadae kuonyesha kiasi cha point kwenye programu hiyo ili kuwezesha ushindani baina ya marafiki wanaotumia mtandao huo wa Facebook.
Game ambazo kwa sasa unaweza kucheza kupitia programu hiyo ya Facebook Messenger ni pamoja na Pac-Man, Space Invaders, Galaga na Words With Friends, ambazo zote hupatikana kwenye programu hiyo moja kwa moja. Kwa sasa sehemu hiyo mpya itapatikana kwenye toleo jipya la programu ya Facebook Messenger na sehem hiyo imepewa jina la Instant Games.
Pia unaweza kucheza game hizo moja kwa moja kwenye sehemu ya News Feed, kumbuka pia kama bado hujapata toleo jipya la Facebook messenger download sasa kupitia Play Store au App Store ili kucheza game hizo.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania tech kila siku au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.