in

Programu ya Facebook Event yaja Rasmi Kwenye Android

Hatimaye programu mpya ya facebook event yaja rasmi kwenye mfumo wa Android leo

Programu mpya kutoka kampuni ya Facebook, Facebook Event leo imezinduliwa rasmi kwenye mfumo wa android. Programu hiyo ambayo ilitangazwa kuja rasmi kabla ya mwisho wa mwaka huu 2016 leo imetangazwa kuwa kwa sasa tayari iko kwenye soko maarufu la Play Store.

Hata hivyo programu kwa mfumo wa iOS ilifanikiwa kutoka ya kwanza kabisa mwezi October na tayari kwa sasa inadownload zaidi ya milioni 100. Facebook Event ni programu inayokusaidia kuangalia mambo mbalimbali yalioko karibu na mahali ulipo kwa kuzingatia tarehe.

Unaweza ukawa wakwanza kujaribu programu hii mpya kwa kudownload kupitia Play Store au unaweza kubofya hapo chini na utapelekwa kwenye soko la Play Store ili kudownload moja kwa moja.

Facebook Local
Price: Free

Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.

Hizi Hapa Apps Nzuri Kwaajili ya Watafutaji wa Ajira Rasmi
Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.