Deki ya Kwanza ya Video Kaseti Ilikua na Ukubwa wa Kinanda

Deki ya kwanza ya video kaseti ambayo ilitengenezwa mwaka 1956 ilikua ni kubwa wa size ya kinanda kikubwa
Deki Deki

Kazi kamili ya kutengeneza deki za video kaseti VCR (video cassette recorder) mwanzoni ilianza rasmi kama videotape recorder (VTR), kazi hii ilikamilika mwaka 1952 kwa mujibu wa Massachusetts Institute of Technology ambapo hapo ndipo ilipo gunduliwa deki hiyo ambayo iligunduliwa na the Ampex Corporation chini ya Charles Ginsburg anae julikana sana kwa sasa kama “father of the video cassette recorder“.

April 14, 1956 Ginsburg pamoja na timu yake walifanikiwa kutengeneza VCR hiyo ya kwanza ya Ampex VRX-1000 ambayo ili kuwa ikiuzwa kwa dollar za marekani $50,000 sawa na shilingi za sasa za Tanzania Tsh 110,000,000. Mafanikio hayo yalisababisha baadhi ya steshei nyingi za televisheni kununua deki hiyo ili kuweza kurekodi vipindi na kuvirudia baadae.

https://www.youtube.com/watch?v=sAXFkRCWhWQ

Advertisement

Baadae kampuni ya RCA na Ampex ziliamua kuungana ili kutengeneza deki kwaajili ya matumizi ya nyumbani na hii ili sababisha ushindani ambapo mwaka 1964 Sony ilifanikiwa kuwa ya kwanza kutoa deki yake kwaajili ya matumizi ya nyumbani na baadae kufuatiwa na kampuni ya RCA na Ampex ambayo ilitoa deki yake baada ya kampuni ya Sony.

Hadi kufikia mwaka 1970 kulikua na deki za aina tatu ikiwemo Betamax (kutoka Sony), VHS (kutoka JVC) na V2000 (kutoka Phillips). Baada ya kipindi kirefu cha ushindani wa kampuni hizi VHS iliweza kushinda ushindani huo baada ya kuleta kaseti zenye uwezo wa kurekodi kwa muda mrefu, hata hivyo VHS iliweza kuendesha soko la video hadi kufikia mwaka 2000 mwaka ambao DVD zilipoingia na kuchukua soko zima la VHS (video cassette recorders).

Na hiyo ndio historia fupi ya deki ya video kaseti (VCR) kuanzia mwaka 1952, kama unataka kujua mambo mbalimbali ya Historia ya teknolojia endelea kutembelea Tanzania tech kila siku au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use