Sasa Tumia Programu ya Chrome ya Android Bila Internet

Toleo jipya la programu ya Chrome kwaajili ya Android linakuwezesha kutumia programu hii bila internet
chrome chrome

Toleo jipya la programu maarufu ya Android (Chrome) linakuja na uwezo mpya wa kuwezesha kutumia programu hiyo bila internet, toleo hilo jipya lenye namba za toleo (Version 55) linakuja kwenye soko la Play Store hivi karibuni likiwa na sifa nyingi mpya tofauti na visakuzi vingine.

Toleo hilo jipya la programu hiyo ya Chrome au (Google Chrome) litakuwezesha kudownload page zote unazotaka kuangalia kwenye simu yako na baadae kukupa uwezo wa kuzipitia page hizo bila kutumia internet. Vilevile toleo hilo la 55 linakuwezesha kushare page hizo na watu mbalimbali ikiwemo pia picha, muziki pamoja na video zilizoko kwenye page hiyo.

Kama mpaka sasa bado huna toleo jipya la programu hiyo kwaajili ya simu yako ya Android, unaweza kudownload kwa kubofya hapo chini.

Advertisement

Google Chrome
Price: Free

Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use