in

Jinsi ya Kuangalia Video za Youtube Kwenye Programu ya VLC

Kama unataka kujifunza namna ya kuangalia video za mtandao wa Youtube kwenye programu ya VLC fuata hatua hizi

VLC

Kuna wakati unakuta unataka kuangalia video za mtandao wa Youtube kwa utulivu bila video hizo kuwa na matangazo au kukata kila mara kwa kuingiliwa na matangazo hayo ambayo ukweli kuna wakati matangazo hayo huwa yanasumbua sana. Pia kuna wakati unakuta unataka kuangalia video za youtube zaidi ya mara moja bila video hiyo kurudia kutumia internet kila mara unapotaka kuangalia tena hapo hapo. Basi kama wewe ni mmoja wa watu wanotaka kufurahia video za mtandao wa youtube kwa urahisi basi endelea kusoma makala hii.

Basi kwa kuanza ni lazima uhakikishe unatumia kompyuta ili uweze kufanikisha kuangalia video za Youtube kwa kutumia programu ya VLC. Kwa kufanya hivyo hakikisha unadownload programu ya VLC kwenye kompyuta yako kama bado hauna programu hiyo, kama unayo programu hiyo basi endelea na hatua zinazofuata hapo chini.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kama tayari umesha download na kuinstall programu ya VLC hatua inayofuata washa programu yako ya VLC kisha bofya kwenye sehemu iliyo upande wa kushoto juu iliyoandikwa Media kisha bofya sehemu ya chini iliyoandikwa Open Network Stream.. baada ya hapo fungua mtandao wa youtube kisha copy link ya video unayotaka kuangalia alafu paste kwenye sehemu iliyoandikwa Please Enter Network URL baada ya hapo bofya kitufe cha Play kilichoko chini upande wakulia kwenye box hilo.

Kwa kufanya hatua hizo utakua umeza kuangalia video za Youtube kwa kutumia programu yako ya kompyuta ya VLC. Kumbuka kuwa video zinazoweza kuPlay kwenye programu hii ni sile ambazo haziko private hivyo ni vizuri kukumbuka hilo wakati unataka kuplay video za Youtube kwenye programu yako ya VLC, pia kuna wakati programu hiyo huwa slow kidogo kusoma video hizo hivyo ni vizuri kuwa na subira kidogo au kama unataka ni vyema kuangalia kwa kutumia kisakuzi (Browser) yako uku ukifuata hatua za jinsi ya kuangalia video za youtube kwa haraka bila kukata.

Kama una maoni au una kitu cha kuongezea unaweza kutuandikia hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Jinsi ya Kuangalia Video za Youtube Kwenye Programu ya VLC
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.