Mpaka sasa tumesha sikia mengi kuhusu simu mpya ya Samsung Galaxy S8, simu hiyo ambayo inatarajiwa kutoka hapo mapema Feb mwaka 2017 imekuwa ni gumzo sana, kutokana na hilo Tanzania tech tunakuletea mambo yote unayo takiwa kuyajua kuhusu simu hiyo ya Samsung Galaxy S8.
- Tarehe ya Kutoka kwa Samsung Galaxy S8
Tetesi kutoka katika tovuti ya Techradar zinasema kuwa simu hiyo inategemewa kutoka tarehe 26 February mwaka ujao yani 2017, simu hiyo inategemewa kuzinduliwa kwenye mkutano wa Mobile World Congress au MWC utakao fanyika huko nchini Barcelona (Kumbuka hizi ni tetesi tu).
- Muundo wa Nje wa Samsung Galaxy S8
Simu hii inategemewa kuja na maboresho ya hali ya juu kuanzia kioo mpaka muundo mzima wa simu hiyo, Simu hii inategemewa kuja na kioo chenye teknolojia ya 4K kikiwa na ukubwa wa inch 5.1 na inch 5.5. Pia tetesi zinasema kuwa simu hii mpya itakuja kwa matoleo mawili ambayo yote yatakuja yakiwa na vioo vya kujikunja au curved screens hata hivyo tetesi kutoka tovuti ya SamMobile zinasema matoleo hayo yatapewa majina ya Dream na Dream 2. Simu hii pia inategemewa kuja na kioo ambacho kitakua karibia asilimia 90 ya muundo wote wa mbele wa simu hiyo (Kumbuka hizi ni tetesi tu).
- Muundo wa Ndani wa Samsung Galaxy S8
Muundo wa ndani wa simu hii unategemewa kuboreshwa zaidi kwa mujibu wa tovuti ya Techradar, RAM ya simu hii inategemewa kuwa GB 6 na Processor ya Snapdragon 830 pamoja na kamera mbili za nyuma moja zikiwa na Megapixel 30 au 12MP, kamera ya mbele au selfie kamera itakuja na Megapixel 8. Pia vilevile simu hiyo inategemewa kuja na projector ndogo ambayo itakuwa nyuma ya simu hiyo karibia na kamera (Kumbuka hizi ni tetesi tu).
Video ya makisio jinsi Samsung Galaxy S8 itakavyokua
Hii ni video ya makisio iliyotengenezwa na Techradar ikiwa inaonyesha jinsi simu hiyo inavyotarajiwa kuwa pale itakapotoka. Kumbuka video hii inaonyesha makisio tu ya simu hiyo hivyo inawezekana simu hiyo isiwe na muonekano huo.
- Battery ya Samsung Galaxy S8
Tetesi kutoka katika tovuti ya Techradar zinasema kuwa simu hii mpya ya galaxy s8 inategemewa kuja na battery yenye uwezo wa 4200mAh ikiwa na uwezo wa kukaa na chaji zaidi ya siku mbili (inategemea na matumizi yako lakini kumbuka hizi ni tetesi tu).
- Bei ya Samsung Galaxy S8
Simu hiyo mpya pia inategemewa kuuzwa kwa kati ya dollar za marekani $850 au Euro£655 AU$1120 (Kumbuka hizi ni tetesi tu).
Hizo ndio baadhi ya Tetesi za simu hiyo ya Samsung Galaxy S8 inayotarajiwa kutoka mwezi february mwaka ujao yani 2017. Tutaendelea kutoa habari mpya za tetesi za simu hiyo kupitia post hii hivyo endelea kutembelea post hii au unaweza kujiunga na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja Youtube kwa habari zote mpya za simu hiyo ya Samsung Galaxy S8. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.