Tovuti Maarufu ya Muziki ya Torrent What.cd Yafungiwa

Soma hapa habari kuhusu tovuti nyingine tena ya muziki ya Torrent kufungiwa
What.cd What.cd

Tovuti ya Muziki ya What.cd ambayo inatumia mfumo wa Torrent hivi karibuni imefungwa na serikali ya ufaransa kwa kuvunja sheria ya hati miliki kwa kusambaza miziki mbalimbali kinyume na sheria.

Tovuti ya What.cd ilianzishwa mwaka 2007 baada ya tovuti nyingine ya muziki ya torrent Oink kufungiwa hapo mwaka 2007. Tovuti ya Oink ilifanikiwa kuwa hewani kuanzia mwaka 2004 mpaka 2007 na kufungiwa rasmi na kupelekea tovuti ya What,cd kuzaliwa rasmi mwaka huohuo 2007. Hata hivyo tovuti ya What.cd ambayo ilikua na Server zake zaidi ya 12 imeondolewa rasmi hapo juzi ambapo kwa sasa tovuti hiyo haipo kabisa.

Mwanzoni baada tu ya kufungiwa tovuti hiyo iliandikwa kwenye ukurasa wake wa mwanzo kuwa tovuti hiyo imeondolewa kabisa na hakutakua na uwezekano wa tovuti hiyo kurudishwa tena kwenye mtandao. Hii ni mara ya tatu sasa kwa mwaka huu kwa tovuti za torrent kufungiwa kutokana na kuvunja sheria za haki miliki, kwani mapema mwaka huu tovuti maarufu ya Kickass torrent nayo ilifungiwa na kufuatiwa na tovuti nyingine ya Torrentz zote zikiwa zinatumia mfumo wa torrent.

Advertisement

Kwa taarifa zaidi za kuhusu tovuti hizi na nyingine nyingi endelea kutembele tovuti ya Tanzania tech kila siku au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use