Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Ndio Simu Zitakazo Pata Toleo Jipya la Android Nougat

Kama ulikua unataka kujua kama simu yako itapata toleo jipya la Android Nougat 7.0 basi hii ndio list ya simu hizo
Android Nougat 7.0 Android Nougat 7.0

Kama wewe unatumia simu yenye kutumia mfumo wa Android lazima utakuwa unajua kuwa Google wametoa mfumo mpya wa Android Nougat 7.0 ambao unategemewa kuja kwenye baadhi ya simu hivi karibuni.

Na hakika hakuna mtu asiependa muonekano mpya wa simu yake baada ya kuitumia zaidi ya miezi sita au hata mwaka ndio mana Android Nougat 7.0 inakuletea muonekano mpya na maboresho mengi ambayo yatafanya simu yako kuwa bora sana kwa upande wa Hardware pamoja na Software.

Advertisement

Kwa kusema hayo basi najua lazima utakua unajiuliza kama simu yako itapata toleo hilo jipya, kama ulikua unajiuliza basi ifuatayo ni list ya baadhi ya simu zitakazo pata toleo hilo jipya la Android Nougat 7.0

Simu Kutoka Kampuni ya Google

Kwa upande wa simu zinazotengenezwa na kampuni ya Google hizi ndio simu ambazo zitapata Toleo jipya la Android Nougat 7.0

  • Nexus 6
  • Nexus 5X
  • Nexus 6P
  • Nexus 9
  • Nexus Player
  • Pixel Series (tayari toleo hilo lipo kwenye simu hizi)

Simu Kutoka Kampuni ya Samsung

Kwa simu za samsung hizi ndio baadhi ya simu zitakazo pata toleo jipya la Android kabla ya mwisho wa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka 2017.

  • Galaxy S7
  • Galaxy S7 edge
  • Galaxy Note 5
  • Galaxy S6
  • Galaxy S6 edge
  • Galaxy S6 edge+

Simu Kutoka Kampuni ya LG

Kama wewe unatumia moja kati ya simu hizi kutoka LG tegemea kupata toleo jipya la Android hivi karibuni.

  • LG V20
  • LG V10
  • LG G5
  • LG G4
  • LG G3

Simu Kutoka Kampuni ya Motorola

Motorola nayo haijasaulika kama unatumia moja kati ya simu hizi baada ya siku chache angalia update kwenye simu yako unaweza kupata toleo hilo jipya la Android.

  • Moto G (4th Gen)
  • Moto G Plus (4th Gen)
  • Moto G Play (4th Gen)
  • Moto X Pure Edition (3rd Gen)
  • Moto X Style
  • Moto X Play
  • Moto X-Force
  • Moto Z
  • Moto Z-Droid
  • Moto Z Force Droid
  • Moto Z Play
  • Moto Z Play Droid
  • Droid Maxx 2
  • Droid Turbo 2

Simu Kutoka Kampuni ya Sony

Kama wewe ni mpenzi wa simu za Sony na unatumia moja ya simu zifuatazo basi furaha kwako kwani simu yako itapta toleo jipya la Android 7.0

  • Xperia Z3+
  • Xperia Z4 Tablet
  • Xperia Z5
  • Xperia Z5 Compact
  • Xperia Z5 Premium
  • Xperia X
  • Xperia XA
  • Xperia XA Ultra
  • Xperia X Performance

Simu Kutoka Kampuni ya HTC

Kwa upande wa HTC pia hizi ndio simu zitakazopata toleo jipya la Android N au Android Nougat 7.0

  • HTC 10
  • HTC One M10
  • HTC One M9
  • HTC One A9

Basi hiyo ndio list ya baadhi ya simu ambazo zitapata toleo jipya la Android Nougat 7.0. Kumbuka kuangalia update kwenye simu yako mara kwa mara au weka Automatic kwenye simu yako kama umeona simu yako iko kwenye list hiyo hapo juu.

Kwa kupata habari zaidi kuhusu toleo hilo jipya endelea kutembelea Tanzania tech kila siku au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use