Microsoft Yaleta Programu Mpya ya Android ya Microsoft Selfie

Kama wewe ni mmoja wa watu wanapenda picha hasa selfie basi jaribu programu hii mpya kutoka microsoft ya Microsoft Selfie
microsoft-selfie microsoft-selfie

Kampuni ya teknolojia ya microsoft hivi karibuni kupitia programu ya Play Store imetoa programu yake mpya kwaajili ya picha iitwayo Microsoft Selfie. Programu hiyo inayokupa uwezo wa kubadili picha zako na kuwa bora zaidi kwa sasa inapatikana Play Store kwaajili ya Kudownload.

Programu hii inatumia teknolojia ya Microsoft’s experience machine ambayo inakusaidia kufanya picha zako kuwa bora na zinazovutia, programu hii pia inauwezo wa kuweka picha kutoka kwenye kamera moja kwa moja na hata pia kutoka kwenye Gallery ya simu yako. Kama unataka kujaribu programu hii mpya kutoka Microsoft unaweza kubofya hapo chini au unaweza kuitafuta moja kwa moja kupitia Play Store.

Microsoft Selfie
Price: Free

Programu hii imeonekena kufanya vizuri kwa upande wa iOS toka ilipozinduliwa hapo December 2015 nasasa programu hii imekuja rasmi kwenye Android. Je Nini maoni yako kuhusu programu hii mpya ya Android ya Microsoft Selfie.? Unaweza kuandikia maoni yako hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use