Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Programu Bora Kwaajili ya Kufuatilia Michezo ya Mpira wa Miguu

Kama wewe ni mfuatiliaji Mzuri wa michezo basi hizi ndio kati ya programu bora ambazo ni muhimu kuwa nazo
michezo michezo

Najua kama unasoma makala hii basi ni lazima wewe ni mmoja kati ya watu ambao ni wafuatiliaji wazuri sana wa michezo na zaidi zaidi mpira wa miguu. Ukweli ni kwamba kwa Tanzania hapa tuna bahati ya kuwa na channel za michezo lakini tatizo ni kwamba haiwezekani kuwa unafuatilia channel hizi kila mara kwani kuna wakati wa kazi ambapo hapa unakuwa huna nafasi na TV, lakini unaonaje ukiwa na programu kwenye simu yako ambazo programu hizi zitakuwezesha kupata taarifa za michezo hasa za mpira wa miguu muda wowote wakati wowote.

Programu hizi ni rahisi kutumia na zina uwezo mkubwa wa kukupa taarifa mbalimbali za michezo hata kama unataka taarifa za timu fulani pekee, pia kingine kizuri kuhusu programu hizi zina pewa support kubwa na tovuti zao hivyo kama unataka habari zingine za michezo unaweza kupitia tovuti za programu hizo.

Advertisement

Basi moja kwa moja twende tukaanza kuangali programu hizi kumbuka programu hizi hazijapangwa kwa namba bali hizi ndio kati ya programu ambazo zinaonekana kufanya vizuri katika kutoa taarifa za michezo hasa za mpira wa miguu.

Onefootball Live Soccer Scores – Android

Onefootball Live Soccer Scores – iOS

Programu ya Onefootball Live Soccer Scores inakupa uwezo wa kufuatilia mpira wa miguu moja kwa moja kutoka uwanjani, programu hii ina uwezo wa kukupa taarifa za ligi karibia 200 ikiwa ni pamoja na Premier League, Liga MX, Primera Division na nyingine nyingi. Programu hii inakuja kwenye mifumo yote mawili ya iOS na Android pia inapatikana kwenye tovuti yake ya onefootball.com

Soccer Scores FotMob – Android

Soccer Scores FotMob – iOS

Programu hii ya Soccer Scores FotMob inakupa uwezo wa kusoma habari mbalimbali mpira wa miguu kote duniani, programu hii ni moja kati ya programu inayopendwa sana na inauwezo wa kukupa habari za timu yoyote pendekezi pamoja na ligi kubwa mbalimbali. Programu hii inakupa taarifa za ligi kama Premier League, La Liga (Liga BBVA), MLS (Major League Soccer), Europa League, Champions League, Eredivisie, Bundesliga, Serie A, World Cup 2018 na Liga MX pamoja na nyingine nyingi, pia programu inakupa taarifa za soka kupitia kwenye tovuti ya Fotmob.com

Goal.com – Android

Goal.com – iOS

Programu ya Goal.com ni moja ya programu za siku nyingi ambayo sasa imeboreshwa zaidi ambapo sasa inakuletea habari zote za michezo iwe ni kununuliwa kwa mchezaji kuuzwa au habari zote za tetesi programu hii ni bora sana kwako, zaidi programu hii inakupa uwezo wa kupata habari hata za ligi za Tanzania. Programu hii pia inapatika kwenye mifumo yote miwili ya Android na iOS, pia unauwezo wa kupata habari zaidi za soka za nje na ndani ya Tanzania kwa kupitia tovuti yake ya Goal.com

Na hizo ndio programu ambazo ukiwa nazo nahakika lazima utakuwa unapata taarifa zote za michezo hasa za mpira wa miguu, kama unahisi kuna programu tumeisahau usisite kutuandikia kwenye maoni hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use