Programu ya Instagram Kuongezewa Sehemu Mpya ya Live Video

Hivi karibuni kampuni ya facebook kupitia programu yake ya Instagram imetangaza rasmi kuleta sehemu mpya ya Live Video
instagram instagram

Kampuni ya Facebook kupitia mtandao wake wa Instagram hivi karibuni imethibitisha kuwa inafanyia kazi toleo lake jipya la program ya Instagram ili kuleta sehemu mpya ya Live Video.

Kiongozi (CEO) wa Instagram Kevin Systrom alidhibitisha hayo kwenye mahojiano yaliyofanyika na mtandao wa Financial Times wa nchini marekani. Kevin alisema kuwa sehemu hiyo mpya ya live video itafanya programu ya instagram kuwa programu bora zaidi na anaamini italeta ukaribu zaidi baina ya watu na watumiaji wa mtandao Instagram kwa ujumla.

Hata hivyo Kevin hakutoa maelezo zaidi kuhusu sehemu hiyo mpya ya live video jinsi gani itakavyofanya kazi, lakini kwa juhudi binafsi Tanzania tech imefanikiwa kupata picha za monekano wa sehemu hiyo ambapo video ambazo zitakuwa Live zitakuwa zikionekana kwa juu kwenye sehemu ya “stories” ambapo video zitakazo kuwa ziko live zitaonekana na nembo ya neno LIVE.

Advertisement

istagram-live
Picha Kutoka Tovuti ya T Journal ya Urusi

Bado haijajulikana kuwa sehemu hiyo mpya itakuja lini lakini ni uhakika kwamba sehemu hiyo mpya inakuja hivi karibuni kwenye programu hizo za Instagram za Android pamoja na iOS pengine hata kwa wale wanaotumia kompyuta.

Kama unataka habari zaidi kuhusu sehemu hii mpya jinsi endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

2 comments
    1. Sehemu hiyo ipo kwa karibia kila mtu ila kama akaunti yako ni mpya unaweza usione sehemu hiyo kujua jinsi ya kutumia tafuta hapa kwenye tanzania tech kwa kuandika “jinsi ya kutumia Insta live”

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use