Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Download iOS 10.1.1 Hapa kwa Ajili ya iPhone, iPad na iPod Touch

Kama ulikua uatafuta toleo jipya la iOS kwaajili ya iPhone, iPad au iPod Touch download hapa toleo hilo la 10.1.1
iOS 10 iOS 10

Kama wote tunavyojua Apple hivi karibuni ilitangaza kutoa toleo lake jipya la mfumo wa uendeshaji yaani iOS 10, toleo hilo jipya kwa sasa lipo karibia kwenye kila kifaa yani kwa namna moja ama nyingine lazima kama wewe ni mtumiaji wa iPhone, iPad au iPod Touch utakuwa umesha ona simu yako ikionyesha kama kuna toleo hilo jipya.

Najua kuna wakati network inakua slow sana mpaka unajikuta kudownload kitu cha GB 1 au zaidi inakua ni mthiani ndio maana leo tunakuletea namna hii rahisi ya kuinstall iOS 10 kwenye kifaa chako kwa haraka zaidi hata kama uko kwenye eneo lenye Network ndogo.

Advertisement

Kwa kuanza basi hakikisha unatumia kompyuta iwe ni laptop au hata desktop, pia vilevile hakikisha kompyuta hiyo inayo programu ya IDM (Internet Download Manager) kama hauna program hii unaweza kuidownload kupitia hapa, hakikisha umefuata maelekezo yote na install programu hiyo kwenye kompyuta yako. Baada ya hapo angalia aina ya kifaa unachotumia kisha download toleo hilo jipya kwa kutumia link hapo chini

Baada ya kumaliza kudownload hakikisha unayo programu ya iTune kwenye kompyuta yako kwani ili update hizi ziweze kufanya kazi nilazima ziangaliwe kupitia server za apple hivyo ni lazima kuwa na programu ya iTune. Baada ya kuhakikisha programu hiyo ipo kwenye kompyuta yako basi endelea kwa kuchomeka kifaa chako subiri mpaka kifaa chako kionekane kwenye programu ya iTune kisha utaona meseji yenye maneno yakiwa yanakueleza kuwa simu yako au kifaa chako kinaitajika kuekewa toleo jipya.

Ukiona maneno hayo shikilia SHIFT kwenye keyboard yako kisha bofya update (hakikisha huachi shift) moja kwa moja chagua mahali ulipohifadhi file ulilo download awali kisha bofya open. Baada ya hapo acha programu hiyo ya iTune itanza kuangali file hilo kwenye server na baadae simu yako au kifaa chako kitanza ku-update moja kwa moja.

Kama makala hii imekusaidia share na wengine pia unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use