Haya Ndio Mambo Unayotakiwa Kujua Kuhusu Simu za Google Pixel

Haya ndio mambo muhimu unayotakiwa kujua kuhusu simu mpya za Google Pixel
Google Pixel XL Google Pixel XL

Hapo jana kampuni ya Google ilifanya uzinduzi rasmi wa simu zake mpya za Google Pixel pamoja na Google Pixel XL, Google Pixel ni moja ya kati ya simu pekee ambazo zimewahi kutengenezwa kila kitu (Hardware na Software) na kampuni hiyo maarufu ya teknolojia duniani, Hata hivyo uzinduzi huo ulifanyika baada ya kampuni hiyo kuamua kuachana na simu zake za awali za Google Nexus.

Nexus ni simu zilizokua zinatengenezwa na kampuni ya Google kwa kushirikiana na makampuni mengine kama HTC, Huawei na baadhi ya makampuni mengine makubwa duniani yanayo jihusisha na utengenezaji wa simu janja za mkononi yani Smartphones, lakini hadi kufikia hapo jana simu hizo zenye majina hayo ya Nexus kutoka kampuni ya Google zitakuwa zimefikia mwisho wake rasmi yaani hapa nikiwa na maana kuwa simu hizo hazito tengenezwa tena na kampuni hiyo maarufu ya Google badala yake sasa zitakuwa ni simu hizo mpya za Google Pixel ambazo zitakuwa zimebeba kila kitu kutoka kampuni ya Google kuanzia muundo (Hardware) mpaka mfumo wa uendeshaji yani (Software).

Kama hukuweza kuangalia mkutano wa uzinduzi wa simu hizo hapo jana yafuatayo ni mambo muhimu yaliyotangazwa kuhusu simu hizo mpya za Google Pixel na Google Pixel XL.

Advertisement

https://www.youtube.com/watch?v=-S4HqCzyGi0

Nakama ukweza kuangalia video hiyo vizuri unaweza kubofya Hapa ili kusoma sifa za simu hizo mpya za Google Pixel pamoja na Google Pixel Xl.

Ili kupata habari mbalimbali za teknolojia endelea kutembelea blog ya Tanzania tech au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  kwenye simu yako ya Android, au pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.

6 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use