Yote Unayotakiwa Kujua Kuhusu Kompyuta Mpya za MacBook Pro

Haya ndio mambo unayotakiwa kuyajua kabla ya nunua kompyuta mpya za MacBook Pro zilizo zinduliwa rasmi hapo jana
MacBook Pro MacBook Pro

Kama ulikosa kuangali jana Event ya uzinduzi wa kompyuta mpya za MacBook usiwe na wasiwasi kwani yafuatayo ndio mambo ya muhimu unayotakiwa kuyajua kuhusu kompyuta hizo mpya za MacBook Pro zilizo zinduliwa rasmi hapo jana.

Baada ya takriban miaka kadhaa imepita tangu Apple walipotoa toleo jipya la kompyuta za MacBook Pro na siku ya jana kampuni hiyo ilifanikiwa kutoa tena toleo lake jipya lenye baadhi ya mabadiliko. Tofauti na laptop za miaka ya nyuma Apple sasa wanakuletea MacBook nyembamba zaidi na nyepesi zaidi, pamoja na teknolojia mpya za Touch ID pamoja na Touch Bar.

  • Sifa za MacBook Pro Inch 15 yenye Touch Bar

MacBook Pro ya inch 15 itakuwa na uzito wa kg 1.83 ambayo itakuwa imepungua g200 ukilinganisha na MacBook Pro yazamani. Pia kompyuta hizo zitakuwa zikiendeshwa na Processor ya Intel Core i7 yenye uwezo wa 2.6GHz/ 2.7GHz quad-core ikiwa na sehemu mpya ya Touch ID pamoja na Touch Bar. Kompyuta hiyo mpya ya MacBook Pro ya inch 15 itakuwa ikiwezeshwa na RAM ya 8GB pamoja na Hard Disk ya 256GB/512GB yenye kutumia teknolojia ya Hard Disk ya SSD na kwa upande wa Graphics kompyuta hii mpya inayo Graphics ya Intel HD Graphics 530 ikiwa na mfumo wa uendeshaji wa Mac OS Sierra. MacBook Pro ya Inch 15 inakaa na chaji kwa Masaa 10 na kuendela hivyo ni safe kutembea na kompyuta yako bila chaja.

Advertisement

https://www.youtube.com/watch?v=4BkskUE8_hA

  • Sifa za MacBook Pro Inch 13 yenye Touch Bar

Kwa upande wa MacBook Pro ya Inch 13 yenye Touch Bar itakuja na kioo cha inch 13 chenye resolution ya 2560 x 1600 pixels pamoja na 2.9 GHz dual-core Intel Core i5 processor ikiwa na Graphics ya Intel Iris Graphics 550 kompyuta hiyo pia itakuja na RAM ya 8GB ikiwa na Hard Disk ya 256GB/512GB ikiwa na teknolojia ya Hard Disk ya SSD. Pia kompyuta hii inasemekana kukaa na chaji kwa masaa 10 (ila sina uhakika katika hili).

  • Sifa za MacBook Pro Inch 13 isiyo na Touch Bar

MacBook Pro Inch 13 isiyo na Touch Bar haitofautiani sana sifa na ile yenye Touch Bar kwani tofauti kubwa iliyopo ni kwamba kompyuta hii aina Touch Bar na Bei yake ni rahisi kidogo kuliko ile yenye Touch Bar ila kwa sifa zote zinayo Intel Core i5 processor, Graphics ya Intel Iris Graphics 550, ya 8GB ikiwa na Hard Disk ya 256GB/512GB ikiwa na teknolojia ya Hard Disk ya SSD pamoja na Masaa 10 ya chaji.

https://www.youtube.com/watch?v=RDpOB-OXypQ

  • Bei za MacBook Pro Mwaka Huu

Kuhusu Bei za kompyuta hizi MacBook Pro ya inch 15 zitakuja za aina mbili (zote zina Touch Bar) ambazo zitauzwa kwa kati ya dollar za marekani $2,399 sawa na Tsh 5,300,000 na dollar $2,799 sawa na Tsh 6,200,000. Kwa upande wa MacBook Pro ya Inch 13 nazo zitakuja za aina mbili (zote zikiwa na Touch Bar) zitauzwa kwa Kati ya Dollar za Marekani $1,799 sawa na Tsh 4,000,000 na dollar $1,999 sawa na Tsh 4,400,000. Na kwa MacBook Pro ya Inch 13 (Isiyo na Touch Bar) itakuwa ikiuzwa kwa dollar za marekani $1,499 sawa na Tsh 3,300,000.

Ili kujua zaidi kuhusu Kompyuta hizo mpya za MacBook Pro zilizo zinduliwa jana rasmi tembelea tovuti ya Apple kwa kubofya HAPA

Nini maoni yako kuhusu kompyuta hizi mpya kutoka Apple za MacBook Pro tuandikie maoni yako hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use