in

WhatsApp Kuleta Sehemu Mpya ya Video Call Hivi Karibuni

Programu ya WhatsApp hivi karibuni lnakuja na sehemu mpya yenye kukupa uwezo wa kupiga simu za Video

whatsapp-video-call

Video call katika programu ya WhatsApp ni sehemu ambayo imengojewa kwa muda sana na kama wewe ni mmoja wa watu waliokuwa wanaisubiri basi sehemu hiyo mpya inakuja hivi karibuni. Kwa mujibu wa tovuti ya Android Authority sehemu hiyo mpya ya video call ilianza kupatikana kwa watumiaji wa majaribio wa programu ya WhatsApp yaani (WhatsApp Beta) na sasa sehemu hiyo inakuja kwa watumiaji wote hivi karibuni (inawezekana ndani ya wiki au siku kadhaa).

Sehemu hiyo mpya imekua ikingojewa kwa muda sasa toka tetesi za programu ya whatsapp kuja na video call zilipoanza kusambaa. Hata hivyo WhatsApp Video Call itakuwa inafanya kazi kama ilivyo wakati unapiga simu za kawaida kwenye programu hiyo, ili kutumia sehemu hiyo unatakiwa kubofya kitufe cha kupiga simu kwenye programu hiyo kisha utapata kuchagua kati ya kupiga simu za sauti au simu za video yaani (Video call).

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

whatsapp-video-calling-20

ili kumpigia rafiki yako Watu wote mnapaswa kuwa na toleo jipya lenye sehemu hii mpya, kwa sasa kama wewe na marafiki zako mnataka kujaribu sehemu hiyo mpya mnaweza kujiaribu sehemu hiyo kwa ku-dowbload programu ya WhatsApp ya majaribio (WhatsApp Beta) hapo chini.

WhatsApp beta version 2.16.318

Kwa wale wasio ijua programu ya WhatsApp Beta ni programu kutoka WhatsApp amabayo inakuruhusu kujaribu sehemu mpya za programu hiyo kabla hazijafika kwenye programu ya kawaida ya WhatsApp. Kama unataka kujiunga ili uwe unajaribu sehemu hizo mpya unaweza kujiunga kwa kubofya link hiyo hapo chini kisha jisajili na utakuwa ukitumia WhatsApp Beta kama programu yako ya kawaida uku ukiendelea kujaribu sehemu mpya za programu hiyo.

Join WhatsApp Beta

Ukisha jaribu sehemu hiyo mpya unaweza kutuandikia maoni yako hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

WhatsApp Kuleta Sehemu Mpya ya Video Call Hivi Karibuni
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apps Muhimu kwaajili ya Mwezi wa Ramadhani (2024)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.