Kampuni maarufu ya nchini marekani ya Verizon hivi karibuni imetangaza kwenye baadhi ya magazeti ya marekani kuwa inasubirisha kwa muda ununuzi wa mtandao wa Yahoo ili kufanya uchunguzi wa kina kwenye Mtandao huo. Verizon ilitangazwa rasmi kununua mtandao wa Yahoo hapo mwezi July kwa dollar za marekani $4.83 billion.
Hata hivyo uamuzi wa kampuni hiyo kusimamisha kwa muda ununuzi wa mtandao huo ni baada ya kile kilichofanyiaka miaka miwili iliyopita baada ya mtandao huo wa Yahoo kuwa hacked na baadhi ya email za wateja wa mtandao huo kuuzwa kwa makundi ya watu mbalimbali. Kwa bahati mbaya taarifa hizi hazikuwafikia watumiaji wa mtandao huo hadi kufikia mwaka huu 2017 baada ya kampuni Verizon kutangaza rasmi kutaka kununua mtandao huo.
Mwanzoni mwa mwezi huu ununuzi huo uliingia dosari baada ya kampuni ya Verizon kutaka kupunguziwa kiasi cha dollar za marekani $1 Billion kutokana na Mtandao huo kuficha kitendo hicho ambacho kwa kiasi fulani kimesababishia wateja mtandao huo wa Yahoo kukosa uhaminifu na mtandao huo. Hata hivyo hakuna taarifa zozote zinazo sema kuwa Yahoo ilikubali kupunguza dau hilo kutoka $4.83 billion na kuwa $3.83 billion.
Baada ya uamuzi huo hivi karibuni kampuni ya Verizon ilitoa taarifa nyingine kwenye magazeti ya marekani kuwa inasimamisha kwa muda kununua mtandao huo ili kufanya uchunguzi kama tukio hilo limeadhiri mtandao huo na wateja wake kwa kiasi gani. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye tovuti ya CNET yahoo bado haijasikika ikisema chochote kuhusu uamuzi wa wa kampuni hiyo kusitisha kwa muda ununuzi wa mtandao huo.
Ili kujua hatima ya mtandao wa Yahoo endelea kutembelea blog ya Tanzania tech au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech kwenye simu yako ya Android, au unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.