in

Hii Ndio Simu Mpya ya Nokia D1C Yenye Kutumia Android

Kama wewe ni mpenzi wa simu za nokia kaa tayari kwani simu mpya ya Nokia D1C inaweza kuja hvi karibuni

Kampuni ya Nokia kutoka Finland ambayo hapo awali iliji zolea umaarufu mkubwa kwa kutengeneza smartphone za kwanza hivi karibuni imeibuka tena kwenye tovuti iitwayo Geekbench. Tovuti hiyo ambayo ilielezea ujio wa simu mpya ya Nokia D1C ambayo inasemekana kutumia toleo jipya la Android 7.0 Nougat.

Simu hiyo ambayo inasemekana kutumia Processor ya Qualcomm Snapdragon 430 64-bit Octa-Core 1.4 GHz processor pamoja na RAM ya GB 3 pengine ndio simu ambayo itairudisha tena kampuni hiyo ya Nokia kwenye soko la Smartphone Duniani.

Ikiwa sifa zingine za simu hiyo bado hazijajulikana, wapenzi wa nokia kote duniani wanaonekana kufurahishwa na jambo hilo la kampuni hiyo kutoka Finland kurudi tena na simu yenye kutumia Android, hata hivyo simu hiyo inategemewa kutoka hivi karibuni kati ya mwanzoni au mwishoni mwa mwaka huu.

Ili kujua zaidi kuhusu simu hiyo mpya ya Nokia D1C lini itatoka endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  kwenye simu yako ya Android, au pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A21s
Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 2

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.