Kampuni ya Nokia kutoka Finland ambayo hapo awali iliji zolea umaarufu mkubwa kwa kutengeneza smartphone za kwanza hivi karibuni imeibuka tena kwenye tovuti iitwayo Geekbench. Tovuti hiyo ambayo ilielezea ujio wa simu mpya ya Nokia D1C ambayo inasemekana kutumia toleo jipya la Android 7.0 Nougat.
Simu hiyo ambayo inasemekana kutumia Processor ya Qualcomm Snapdragon 430 64-bit Octa-Core 1.4 GHz processor pamoja na RAM ya GB 3 pengine ndio simu ambayo itairudisha tena kampuni hiyo ya Nokia kwenye soko la Smartphone Duniani.
Ikiwa sifa zingine za simu hiyo bado hazijajulikana, wapenzi wa nokia kote duniani wanaonekana kufurahishwa na jambo hilo la kampuni hiyo kutoka Finland kurudi tena na simu yenye kutumia Android, hata hivyo simu hiyo inategemewa kutoka hivi karibuni kati ya mwanzoni au mwishoni mwa mwaka huu.
Ili kujua zaidi kuhusu simu hiyo mpya ya Nokia D1C lini itatoka endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech kwenye simu yako ya Android, au pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.
Safi sana mi nawapongezeni kwa ukulasa wenu huu
Asante sana jmerciful karibu