Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Ndio Sifa Kamili za Simu Mpya za Google Pixel na Google Pixel XL

Simu hizi za Google Pixel na Pixel XL zinatarajiwa kutoka hapo kesho, lakini hizi ndio sifa kamili za simu hizo
Hizi Ndio Sifa Kamili za Simu Mpya za Google Pixel na Google Pixel XL Hizi Ndio Sifa Kamili za Simu Mpya za Google Pixel na Google Pixel XL

Google inatarajia kuzindua simu zake mbili hapo kesho simu hizo za Google pixel na Google pixel XL zinategemewa kuja na muonekano bora na wakisasa kabisa. Kwa muda sasa zimekua ziki sambaa tetesi mbalimbali juu ya simu hizo kuanzia muonekano mpaka sifa za simu hizo, lakini leo tanzania tech tunakuleta sifa halisi za simu hizo mbili ambazo kwa sasa yamebaki masaa machache kwa simu hizo kuzinduliwa kwenye mkutano utakao fanyika huko San Francisco nchini marekani.

Basi bila kupoteza muda zifuatazo ndio sifa halisi za simu hizo mbili za Google Pixel pamoja na Google Pixel XL.

Advertisement

SIFA ZA GOOGLE PIXEL 

  • Ukubwa wa simu ni : 143.8 x 69.5 x 8.6 mm,
  • Uzito wake ni 143 grams
  • Ukubwa wa kioo ni : inch 5 ikiwa na teknolojia ya Full HD AMOLED, 441 ppi, Gorilla Glass 4
  • Processor ni : 2.15GHz Snapdragon 821 (quad-core, 64-bit)
  • RAM: 4GB
  • Ukubwa wa memory ya ndani : 32GB or 128GB
  • Kamera ya nyuma : 12.3MP, f/2.0, 1.55um, OIS.
  • Kamera ya mbele 8MP
  • Battery: 2,770 mAh, fast charging
  • Sifa zingine ni : fingerprint scanner, USB Type-C, NFC, 3.5 mm headphone jack
  • Mfumo wa uendeshaji OS: Android 7.1

Hizo ndio sifa za simu ya Google pixel, zifuatazo ni sifa za simu nyingine ya Google Pixel XL.

SIFA ZA GOOGLE PIXEL XL

  • Ukubwa wa simu ni : 154.7 x 75.7 x 8.6 mm,
  • Uzito wake ni 168 grams
  • Ukubwa wa kioo ni : 5.5-inch Quad HD AMOLED, 534 ppi, Gorilla Glass 4
  • Processor ni : 2.15GHz Snapdragon 821 (quad-core, 64-bit)
  • RAM: 4GB
  • Ukubwa wa memory ya ndani : 32GB or 128GB
  • Kamera ya nyuma : 12.3MP, f/2.0, 1.55um, OIS
  • Kamera ya mbele 8MP
  • Battery: 3,450 mAh, fast charging
  • Sifa zingine ni : fingerprint scanner, USB Type-C, NFC, 3.5 mm headphone jack
  • Mfumo wa uendeshaji Android 7.1

Kama unataka kujua zaidi kuhusu zimu hizi ambazo zitazinduliwa rasmi hapo kesho pamoja na kuangalia mkutano wa uzinduzi wa simu hizo live kutoka marekani endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  kwenye simu yako ya Android, au pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use