in

Nintendo Switch Kifaa Kipya cha Kucheza Game Kutoka Nintendo

Kama wewe ni mpenzi wa Video game basi huu ndio ujio wa kifaa kipya cha kucheza game kutoka nintendo

Nintendo Switch

Hivi karibuni kampuni ya Nintendo yenye makao makuu huko Kyoto nchini japan ilitangaza kifaa chake kipya kwaajili ya kucheza game, kifaa hicho kilicho pewa jina la Nintendo Switch kilizinduliwa rasmi kwa video maalum ya utambulishi hapo tarehe 20 october mwaka huu.

Nintendo Switch inakuja ikiwa na uwezo wa ziada wa kubadilika na kuwa game maalum ya mkononi au hata ile ya mezani kwaajili ya kucheza kwenye TV yako. Katika video ya utambulishi wa kifaa hicho kipya kutoka Nintendo inaonekana kifaa hicho kipya cha Nintendo Switch kitakuwezesha kuendelea kucheza game unapokua nyumbani au hata pia unapokua umetoka, ili kugeuza game hiyo kuwa ya mkononi unatakiwa kuchomeka vibonyezo viwili maalum (pad) ambavyo vitakuwezesha kuendelea kufurahia kucheza game hiyohiyo ambayo ulikua unacheza nyumbani kwenye TV yako.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Nintendo Switch inategemewa kutoka kuanzia Mwezi April mwaka ujao 2017 lakini Bado mpaka sasa haijajulikana kuwa kifaa hicho kipya kitakuja na game zake pekee au kitakua kinatumia game zingine zilizopo kutoka kampuni hiyo ya Nintendo. Kwa sasa kama unavyoona kwenye video hapo juu Nintendo Switch itakuwa inatumia Memory Card hivyo inawezekana kifaa hicho kuwa na uwezo wa kudownload game zake moja kwa moja kwenye Memory Card.

Ili kujua sifa za Nintendo Switch pamoja na bei yake endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au download App ya Tanzania tech ili uweze kupata habari zote mpya za teknolojia mara tu zinapotoka, pia unaweza kujiunga na mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Nintendo Switch Kifaa Kipya cha Kucheza Game Kutoka Nintendo
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.