in

Google Kuleta Huduma za TV Mtandaoni Ifikapo Mwaka 2017

Kampuni ya teknolojia ya Google imepanga kuleta huduma za bei rahisi za tv mtandaoni ifikapo mapema 2017

TV

Wakati kampuni ya Apple ikiwa imesitisha mpango wake wa kuleta huduma za tv mtandaoni, kampuni maarufu ya teknolojia ya Google hivi karibuni imetangaza kuanza mpango wake wa kuleta tv kwenye mtandao. Mpango huo ambao unategemewa kukamilika katikati ya mwaka 2017 utakuwa ukihusisha baadhi ya televisheni maarufu za michezo, habari na makala kutoka marekani.

Katika kuhakikisha inatoa huduma bora kampuni hiyo imesema kuwa huduma hizo zitakuwa bora na za bei nafuu ambapo inategemea asilimia 80 ya watu wote wataweza kumudu gharama za kuangalia tv hizo. Hata hivyo huduma hiyo inasemekana kutenganishwa kabisa na huduma ambayo ipo kwa sasa kwa upande wa YouTube ijulikanayo kama Youtube Red ambayo kwa hapa Tanzania huduma hiyo bado haijawezeshwa, tayari Google imeshafanikiwa kusaini mkataba na kampuni ya CBS Corp yenye kituo cha televisheni pamoja na channel ya CBS ambayo imesha kubali kuanza kufanya matangazo yake kwenye mtandao huo mpya unaokuja hivi karibuni. Pia inasemekana kuwa Google inaendelea kufanya makubaliano na televisheni nyingine zaidi kama vile 21st Century Fox pamoja na Disney zote kutoka nchini marekani.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Bado mpaka sasa mtandao huo haujajulikana utakua na jina gani ila kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya The Wall Street Journal, mtandao huo mpya kutoka Google unategemewa kuwa wa bei nafuu kuanzia dollar za marekani $25 hadi dollar $40 ambazo ni sawa na Shilingi za kitanzania Tsh 54750.00 hadi 87600.00 kwa mwezi. Hata hivyo bado haijatangazwa kama mtandao huo utakua ukitoa huduma zake Africa, mpaka hapo itakapo julikana tutaendelea kuwahabarisha kuhusu mtandao huo mpya kutoka Google.

Unaweza kuendelea kupata habari za teknolojia kwa kujiunga na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram bila kusahau Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video, Pia kama unataka kupata habari kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na utapata habari zote mpya  pamoja na video pindi tu zinapotoka.

Google Kuleta Huduma za TV Mtandaoni Ifikapo Mwaka 2017
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.