Siku chache zimepita toka Twitter ilipotangaza kusitisha mtandao wa Vine ambao ulinunuliwa na mtandao huo hapo mwishoni mwa mwaka 2012, Twitter iltangaza kuachana na mtandao huo baada ya kuona mtandao huo haufanyi vizuri kwa sasa. Hata hivyo katika taarifa za kuzimwa kwa mtandao huo wa Vine Twitter ilitangaza kuwa tovuti ya Vine itaendelea kuwepo kama kawaida lakini watumiaji hawatokua na uwezo wa ku-upload video za aina yoyote.
Katika muendelezo wa stori hii kampuni pamoja na mtandao wa Giphy umetangaza rasmi kukomboa watu waliokua na akaunti kwenye mtandao huo wa Vine. Giphy ilitangaza kuwa iko mbioni kuachia programu maalum ambayo watumiaji wa vine wataweza kuamisha video kutoka kwenye akaunti zao na kwenda kwenye mtandao huo wa Giphy ambao unajulikana sana kwa kuwa na idadi kubwa ya picha zinazo tembea maarufu kama Gif.
Hata hivyo video zote zilizoko kwenye mtandao huo zitabadilishwa na kuwa picha maalum zijulikanazo kama Gif, vilevile Giphy imetangaza kuhifadhi nakala halisi za video hizo kwenye mtandao wake huo maarufu wa kutafuta picha hizo maarufu kama Gif. Mpaka sasa bado programu hiyo haijatoka rasmi ila kampuni hiyo imesema kuwa programu hiyo inakuja hivi karibuni.
Je unasemaje kuhusu ukombozi huu wa Giphy kubadilisha video zote za Vine na kuwa Gif.? unaweza kuandika maoni yako hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store