Facebook Kuzindua Programu Maalum ya Kuonyesha Matukio (Event)

Facebook imeamua kutengeneza programu maalumu ya Matukio (Events)
event event

Kampuni ya facebook kupitia mtandano wake wa facebook kwa mara nyingine tena imeleta programu yake mpya ambayo itakua ni maalum kwaajili ya Matukio mbalimbali yaani (Event), programu hiyo mpya itakua ikifanya kazi sawa na sehemu ambayo pia inapatikana kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook. Ikiwa na sifa mbalimbali programu hiyo itakusaidia kuona Matukio (Event) mbalimbali ambazo zimeandaliwa na ndugu, jamaa, marafiki au hata sehemu mbalimbali ulizo zifuata (Follow) kwenye mtandao huo wa facebook.

Mbali na hapo programu hiyo inakuwezesha kuona matukio mapya ambayo yapo kwenye eneo maalum ulilopo, kwa mfano kama wewe uko Dar es Salaam basi programu hiyo itakua ikikuonyesha matukio mbalimbali yanayo tarajia kufanyika na yanayofanyika katika mji wa Dar es salaam pamoja na maeneo yote yanayo zunguka mji wa Dar es Salaam.

Advertisement

Kwa sasa programu hiyo inapatikana kwenye mfumo wa iOS lakini pia inatarajiwa kuja hivi karibuni kwenye mfumo wa Android. Hata hivyo kwa mujibu wa maoni ya watumiaji wa programu hiyo kwenye mfumo wa iOS, watu wengi wanaonekana kufurahia programu hiyo mpya kwani wanasema inawarahisishia kuandaa pamoja na kuangali Matukio (Event) mbalimbali kwa urahisi kuliko hapo awali kwenye mtandao huo wa facebook.

Hata hivyo bado haijajulikana tarehe halisi ambayo facebook itatoa programu hiyo kwa watumiaji wake wa mfumo wa Android lakini tunaahidi kukujuza zaidi kuhusu hilo hivyo Ili kujua zaidi kuhusu programu hiyo mpya ya facebook endelea kutembelea blog ya Tanzania tech au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  kwenye simu yako ya Android, au pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use