Kwa sasa kwenye ulimwengu mzima wa televisheni kuna teknolojia nyingi sana kuanzia HDR, 4K, UHD na nyingine nyingi, pengine ulisha wahi kujiuliza nini maana ya maneno hayo au nini maana ya teknolojia hizo.? Kwa muda sasa na uhakika ulisha jiuliza hata mara moja kuwa HDR TV ni nini.? Basi kama ulisha wahi kujiuliza hivyo leo tutaenda kuangallia nini maana ya teknolojia hiyo ambayo ina patika kwenye televisheni mbalimbali za kisasa. Kama unataka kujua kuhusu 4K pamoja na UHD unaweza kutembele makala zetu zingine ambazo tayari tumesha elezea kuhusu teknolojia hizo.
Basi kwa kuanza tujue kwanza ni nini maana ya HDR na utaijuaje televisheni yenye teknolojia ya HDR. Kwa kirefu HDR ni (High Dynamic Range) huu ni ule uwezo wa televisheni kuweza kukoleza rangi nyeusi na nyeupe ili kuwezesha picha kuonekana angavu na kuipa picha nguvu inayotakiwa ambapo ndipo jina (Dynamic) lilipotoka. Televisheni zenye teknolojia hii zinauwezo mkubwa wa kuonyesha picha iliyokolea rangi nyeupe na nyeusi na kuacha rangi zingine zikiwa hivyohivyo bila kubadilika sana. Ukweli ni kwamba rangi kuu katika picha yoyote ni nyeusi na nyeupe hii ni kwa mujibu wa macho yetu wanadamu, kiasi cha rangi nyeupe au nyeusi unachoona ndicho kinakuwezesha kujua kama picha hiyo inaonekana kwa ubora unaotakiwa ama laah.
Kwa kitaalamu ili televisheni iweze kuitwa HDR TV ni lazima ipitie vipimo viwili vikubwa, moja ya kipimo hicho kikubwa ni kupima kiasi cha Mwanga yani (contrast) ambapo hichi ndio kitu kikubwa sana kwenye televisheni yoyote na ndio kikubwa kwenye TV zenye teknolojia ya HDR. Kwa kawaida ili kupima kiasi cha (contrast) au mwanga nilazima hapa televisheni hupitia majaribio ya aina mbili moja ni kupima kiasi cha mwanga yani (peak brightness) ambapo TV hupimwa kiasi cha mwanga inachoweza kutoa na hii hufanyika kwa kupima kiasi cha (Nits) ambazo ni lazima zifikie kiwango kinachotakiwa ili televisheni iweze kuitwa HDR TV. Jaribio la pili ambalo TV zenye teknolojia ya HDR hupitia ni kupima kiasi cha rangi nyeusi yani (black level) vilevile (Nits) hutumika kupima kiwango cha rangi nyeusi kinachoweza kutolewa ambapo nilazima televisheni ifikie kiwango fulani cha (Nits) kinachotakiwa ili televisheni hiyo iweze kuitwa HDR TV. Tofauti kati ya (peak brightness) na (black level) hii kwa kitaalamu ndio huitwa (contrast ratio) ambapo ndio husaidia kupata kiwango cha rangi nyeupe ama (contrast) kwenye televisheni ya HDR.
Kipimo cha pili kikubwa ni lazima televisheni ya HDR kupitia ni kupimwa kiwango cha rangi, hapa televisheni ya HDR inatakiwa kufikisha kiwango flani cha rangi ambacho kitaalamu huitwa 10-bit au (deep colour), hapa ni kwamba hizo (10-bit colour) ni sawa na signal moja yenye mkusanyiko wa rangi tofauti zaidi ya billioni moja. kwa kulinganisha ukiangalia teknolojia ya Blu Ray hii hutumia 8-bit colour ambazo ni sawa na rangi tofauti zaidi ya milioni 16, hivyo basi televisheni ya HDR yenye uwezo wa kuonyesha rangi tofauti zaidi ya bilioni 1 nidhahiri itakuwa na uwezo wa kuonyesha picha angavu zaidi.
Hii haishii hapo pia televisheni ya HDR TV ni lazima iweze kuonyesha kiwango fulani cha kinachojulikana kama (P3 colour) ambapo kiasi hichi hupimwa kwa kuangalia kiwango cha (colour spectrum) au wigo wa rangi. Namna nzuri ya kujua hili ni kwa kufiria labda eneo kubwa lenye mkusanyiko wa rangi nyingi mbalimbali na ndani ya mkusanyiko huo wa rangi (P3 colour) imechukua eneo kubwa la mkusanyiko huo, hivyo kwa kupima ukubwa wa eneo hilo au (colour spectrum) au wigo wa rangi ndipo utaweza kupata kiwango cha (P3 colour).
Kwa Maelezo zaidi tazama video hapo juu na ili kujua zaidi kuhusu televisheni endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech kwenye simu yako ya Android, au pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.