Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuangalia Video za YouTube kwa Haraka Bila Kukata

Kama unataka kuangalia video za Youtube kwenye kompyuta bila video hiyo kuload kila mara (Buffering) fuata hatua hizi
youtube youtube

Wote tunajua kuwa kuna wakati mtu unapata hasira sana pale unapotaka kuangalia video flani kwenye mtandao wa Youtube lakini unakuta video hiyo ina kata kata kila mara kiasi kwamba unaweza kukata tamaa ya kuangalia video hiyo. Basi kama wewe ni mmoja wa watu hao basi leo tunakuletea namna rahisi sana ambayo unaweza kuangali video za youtube bila video hizo Kukata kila mara.

Kwa kuanza basi kumbuka kwa sasa hatua hizi ni kwa wale wanao tumia kompyuta tu, kama unatumia simu endelea kutembelea tovuti ya Tanzania tech kila siku kwani tunaendelea kutafuta namna ya kufanya hatua hizi kwenye simu yako janja aka smartphone. Basi baada ya kusema hayo twende tukaanze moja kwa moja namna ya kufanya video za Youtube kuload kwa haraka na bila ku-kata kata.

Advertisement

Hatua ya kwanza ni kwa wale wanao tumia kisakuzi (Browser) cha Google Chrome, kama unatumia Google Chrome bofya link hiyo hapo chini kudownload Google Chrome Extension ambayo ndio tutatumia kufanya video za youtube kuload bila ku-kata kata.

Download Chrome Extension

Baada ya kudownload na ku-install programu hiyo kwenye kompyuta yako endelea kwa kufuata hautua kwenye video hapo chini.

Hatua ya hii ni kwa wale wanao tumia kisakuzi (Browser) cha FireFox, kama unatumia FireFox bofya link hiyo hapo chini kudownload Google Chrome Extension ambayo ndio tutatumia kufanya video za youtube kuload bila ku-kata kata.

Download Firefox Addon

Baada ya kudownload na ku-install fuata maelekezo kwenye video hapo chini na ukimaliza kuangalia video hiyo utakuwa umewezesha kompyuta yako kustream video za youtube bila ku-kata kata.

Kama mafunzo haya yamekusaidia au kama umekwama sehemu yoyote unaweza kutuandikia maoni yako hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

7 comments
    1. Asante Adam kwa kutembelea Tanzania tech kama unatafuta namna ya kufanya hivyo tumia kibonyezo cha kutafuta kutafuta makala hiyo hapa, unaweza kupata kibonyezo hicho juu kabisa kwenye tovuti hii.

  1. hivi kiongozi samahani nataka kujua nawezaje kuweka maneno kwenye video nitakazo rusha YouTube kama Yale mf.”Kupata hari zaidi usisahau Ku subscriber”
    pia kuweka logo yangu kwenye video husika niliyotuma mf. wako ukituma iwe Tt au kama ITV na n.k

    1. Habari, hiyo inategemeana na aina ya programu unayo tumia ku-edit video zako, sisi tunatumia Adobe Premiere Pro pamoja na Camtasia.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use