Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Twitter Yatoa Link Kwenye Hesabu ya Maneno 140

Baada ya kuondoa picha, sasa link nazo zimeondolewa kwenye hesabu ya maneno 140 ya post za twitter
Twitter-yaondoa link Twitter-yaondoa link

Mtandao maarufu wa kijamii wa Twitter hivi karibuni baada ya kuondoa picha kwenye hesabu ya maneno ya post zake sasa link nazo zimeondolewa kwenye hasabu ya maneno hayo 140.

Kuanzia september 19 mwaka huu 2016 link zitakua hazihesabiwi tena kwenye maneno hayo 140 hivyo hii itakupa nafasi mtumiaji kuweza kuandika maneno mengi zaidi pamoja na link. Hata hivyo mabadiliko hayo yamekuja wakati twitter ikifanya maboresho ya mtandao huo ili kusaidia watumiaji wengi zaidi kufikia ndugu, jamaa, marafiki na hata wateja na biashara mbalimbali.

Advertisement

Hata hivyo ni mapema sana kusema yakuwa twitter itabaki na mfumo huohuo kwani blog mbalimbali za teknolojia nchini marekani zimeandika kuwa kunao uwezekano wa (usernames) pia kutolewa kwenye hesabu ya maneno hayo 140 ya kupost kwenye mtandao huo wa twitter.

Ili kujua habari zaidi kuhusu mtandao huu wa kijamii wa twitter endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use