Sasa Tumia Link Maalum Kualika Watu Kwenye WhatsApp Groups

Sasa Unaweza kualika watu kwenye Group za WhatsApp kwa kutumia link
Groups Groups

Hivi karibuni whatsapp kupitia programu yake ya whatsapp Beta imejitokeza sehemu mpya ambayo groups admin wataweza kualika watu kwenye magroup ya kuchat kwenye programu hiyo ya WhatsApp kwa kutumia link maalum.

Link hiyo maalum itakuwezesha kuwasaidia watu wote wenye link hiyo kuingia moja kwa  moja kwenye group hilo na hakuna haja ya kuwa na namba, vilevile link hiyo inaweza kuondolewa na admin au hata kubadilisha pale admin atakapo ona kuwa inatumiwa vibaya.

Hata hivyo sehemu hiyo mpya bado haijatoka kwenye programu ya kawaida ya WhatsApp bali sehemu hiyo mpya imekuja rasmi kwenye programu ya WhatsApp ya Majaribio ijulikanayo kama Whatsapp Beta. Kama ungependa kujaribu sehemu hiyo mpya unaweza kujiunga na kuwa mmoja kati ya watu watakao kuwa wanajaribu sehemu mpya za programu za WhatsApp kwa kubofya hapo chini kisha download programu hiyo ya WhatsApp Beta.

Advertisement

JIUNGE HAPA

Sehemu hiyo mpya inategemewa kuja hivi karibuni kwenye programu ya WhatsApp hivyo kuwa karibu na simu yako na ukiona simu yako inaonyesha kunazo update za programu hizo za WhatsApp hakikisha una download haraka na utaona sehemu hiyo mpya.

Ili kujua habari zote za programu mbalimbali za teknolojia endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

2 comments
  1. Magembe frank toka Tanga Tanzania Tunashukulu kwa website hiyo inatufahamisha kwa habari nzuri tunashukulu ila jinsi yakuipa link hiyo ya whatsApp ni vipi?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use