Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali, inawezekana simu mpya ya Samsung Galaxy S8 ikaja na sifa bora pengine kuliko simu nyingine zote ambazo zimewahi kutolewa na kampuni hiyo ya Korea kusini.
Tetesi hizo za hivi karibuni zinasema kuwa simu hiyo inayotegemewa kutoka mwaka 2017 itakuwa na kioo kinachotumia teknolojia mpya ya 4K pamoja na kamera ya nyuma yenye uwezo wa 30MP ikiwa na sehemu maalum inayosemekana kuwa ni projector ndogo. Ripoti hizo kutoka kwenye tovuti ya Tech Updates zinaendela kusema kuwa simu hiyo mpya itakuja na kioo chenye inch 5.2 pamoja na resolution ya 2160 x 4096 ikiwa na battery yenye uwezo wa 4200 mAh.
Habari hizo za tetesi zinaendelea kusema kuwa simu hiyo itakua na teknolojia za retina pamoja na fingerprint scanners vyote vikiwa vinaendeshwa na simu hiyo itakayokuwa na memory ya GB 64 au GB 128.
Wakati tetesi hizi zinaonekana kama si zakuamini sana, yote yatadhihirika mwezi February 2017 huko Barcelona kwenye tamasha lijulikanalo kama Mobile World Congress ambapo Samsung ndio itakapo zindua simu yake hiyo ya Samsung Galaxy s 8. Ili kujua zaidi kuhusu tetesi za simu hiyo mpya ya Samsung Galaxy S 8 endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube ili kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.