Google Yapanga Kubadilisha Jina la Simu Zake za Nexus

Kampuni ya Google Yaamua Kuachana na Jina la Simu zake za Nexus
Google yaachana na jina la nexus Google yaachana na jina la nexus

Kwa wale watumiaji wa simu za Google Nexus hii ni taarifa kwenu kwani kampuni maarufu ya teknolojia ya Google imetangaza kuachana na jina la simu zake za Google Nexus, taarifa za kampuni hiyo zimesembaa ziksema kuwa imechukua uamuzi huo na kuwa haito toa tena simu zake za Google Nexus kwa jina hilo la Nexus.

Hata hivyo taarifa hizi bado hazija ongelewa rasmi na kampuni hiyo ya Google lakini taarifa kutoka kwenye blog mbalimbali za teknolojia za nchini marekani zinasema kuwa kampuni hiyo imepanga kubadilisha kabisa muonekano wake kwa upande wa simu hizo za Google Nexus. Hata hvyo inasemekana simu mpya za google zitakuja na muonekano mpya kabisa ambao utafanana na picha hiyo hapo chini japo hakuna uhakika kuhusiana na hilo.

 

Advertisement

Simu Mpya ya Google Nexus

Hata hivyo kubadilika kwa jina hilo la simu hizo ni namna mpya na ujio mpya wa kampuni hiyo maarufu ya Google kwenye upande wa simu zake hizo za Google, ili kupata habari za jina jipya la simu hizo mpya endelea kufuatilia blog yako mpya ya habari za teknolojia ya tanzania tech pia unaweza kupata habari za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa kupakua App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use