Hatimaye Programu ya Google Allo Yatoka Rasmi Leo

Programu Mpya ya Google Allo yatolewa Rasmi leo na Kampuni ya Google
Google Allo Google Allo

Hatimaye kampuni ya Google kupitia blog yake leo imeandika kuwa sasa programu ya Google Allo imetoka rasmi, Programu hiyo ambayo ilitegemewa kutoka wiki hii sasa imetoka rasmi na tayari watu mbalimbali duniani wamesha anza ku-download programu hiyo.

Google Allo ni programu mpya ya kuchat ambayo inakuwezesha kuchat kwa namna ya tofauti na kisasa zaidi kwani programu hiyo inauwezo wa kukupa maoni ni kitu gani cha kujibu pale unapokua unachat, ikiwa na mambo mengine mbalimbali programu hiyo inapatikana rasmi kwa watumiaji wote wa iOS pamoja na Android.

Kama bado hauku pata nafasi ya kudownload programu hiyo usiwe na wasiwasi kwani programu hiyo itakufikia hivi karibuni kwani haiwezekani kufika kwa watu wote duniani kwa mara moja hivyo kama we ni mpenzi wa kuchati usijali programu hiyo itakufikia tu..!

Advertisement

https://www.youtube.com/watch?v=VXEkoXgb4bI

Pia unaweza ukapitia blog ya tanzania tech kila siku au ili kujua kama programu hiyo imekufikia unaweza kujisajili kwa ku-bofya mfumo wa simu yako kama unatumia Android  bofya Android kisha jisajili vilevile kwa iOS fanya hivyo hivyo.

Habari za Hivi Punde 23-09-2016 : Sasa Programu ya Google Allo iko tayari kudownload kwa Tanzania Download Hapa

Mfumo wa Android 

Google Allo
Price: Free

Mfumo wa iOS

Google Allo
Price: Free

Kama unataka kupata habari zaidi za Programu hiyo mpya endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use